Yusuf
Manji ameshinda nafasi ya uenyekiti wa Yanga kiulaini kutokana na
kutokuwa na mpinzani kwenye nafasi hiyo hivyo kupita bila kupingwa
kwenye nafasi ambayo alikuwa akiitetea.
Clemen Sanga nae amepenya katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa kumbwaga mpinzani wake Titus Osoro.
Shughuli pevu ilikuwa kwa wagombea nafasi ya ujumbe ambapo jumla ya wagombea 20 walikuwa wakiwania nafasi 8 za ujumbe.
Mwenyekiti
Yusuf
Manji ameibuka mshindi wa nafasi ya uenyekiti akipenya bila kupingwa na
kupata idadi ya kura 1468 zilizopigwa na wanachama, huku kura 2 pekee
zikiwa zimeharibika.
Makamu Mwenyekiti
Clement Sanga amemgaragaza mpinzani wake baada ya kupata kura 1428 wakati mpinzani wake Titus Osoro akiambulia kura 80 pekee.
Wajumbe
Ayoub
Nyenzi (889), Salim Mkemi (894), Bakar Malima (577), Godfrey Mheluka
(430), David Ruhago (582), Lameck Nyambaya (655), Sylvester Haule (197),
Pascal Laizer (178), Samwel Lukumay (818), Hashim Abdallah (727),
George Manyama (249), Hussein Nyika (770), Siza Lyimo (1027), Beda
Tindwa (452),Tobias Lingalangala (889), Athumani Kihamia (558), Mchafu
Chakoma (69), Edgar W Chibura (72), Ramadhani M. Kampira (182), Omary
S. Amei (1069)
Kwa
Matokeo hayo, uongozi mpya wa Yanga uliochaguliwa na wanachama unaundwa
na Mwenyekiti Yusuf Manji, Makamu Mwenyekiti Clement Sanga huku wajumbe
wakiwa ni Omary S. Amei, Siza Lyimo, Salim Mkemi, Tobias Lingalangala,
Ayoub Nyenzi, Samwel Lukumay, Hussein Nyika na Hashim Abdallah
0 comments:
Post a Comment