Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, mmoja kati ya
viongozi wa juu wa label hiyo, Babu Tale amesema wao kama uongozi
watasimama kidete kuhakikisha wasanii wa WCB wanakuwa mfano wa kuigwa
kwa jamii.
“Nikijibu hapo kwenye eneo la nidhamu ni kwamba, sisi ni vijana
ambao tunaishi na vinaja ambao wametoka kwenye familia zao ambazo
zinamalezi tofauti tofauti, lakini wakija hapa ni lazima wafuate sheria
zetu.
Sitaki kumsifia Dioamond ni mtu ambaye hana nidhamu ya kuigiza, kwa hiyo hawa wengine lazima wafuate tabia za kaka yao,” alisema Babu Tale.
Aliongeza, “Kwetu msanii akitukana kwenye social network ,
akitukana kwenye stage huyo lazima sisi tumuadhibu. Kuna adhabu ambayo
inasukumwa na social network hiyo hatuizingatii kwa sababu kila mmoja
ana mapenzi yake na wengine wanachuki zao.
Adhabu ambayo tatizo
linaonekana wazi kwamba hili ni tatizo, tunayaita matendo kusudi,
kiofisi huwenda mtu akasimamishwa bila jamii kujua, kukata pesa kwenye
kazi zake bila jamii kujua, hayo mambo tunafanyia hata sisi viongozi
pale tunapokosea,
0 comments:
Post a Comment