Wachambuzi
na wadau mbalimbali wametoa maoni yao kuhusu Bajeti ya Serikali kwa
mwaka wa fedha 2016/17, huku watumiaji wa huduma za fedha kwa njia ya
simu wakikumbwa na maumivu wa kodi.
Hiyo
ni siku moja baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango
kuwasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 20116/17.
Pamoja
na mambo mengine, bajeti hiyo inapendekeza kuongeza ushuru wa vinywaji
baridi, maji ya juisi, vinywaji vikali, bia na sigara.
Pia itawagusa watumiaji wa M-pesa, Tigopesa, Airtel Money, Ezypesa kwa kukatwa Sh 280 kwa kila Sh 1000 watakayotuma.
Jana
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), alisema hatua hiyo
ya Serikali kuendelea kutafuta kodi kwa kuzidi kuwaumiza wananchi
inakwenda kinyume na matarajio ya Watanzania wengi.
Alisema
katika bajeti hiyo ya Serikali na ukusanyaji wa mapato yake, katika
kila Sh 1000 itakayokatwa kwa huduma kwenye ATM kuanzia Julai Mosi
mwaka huu, Sh 280 zitachukuliwa na TRA.
Zitto
alisema hali hiyo pia itawakumba watumiaji wa miamala ya M-pesa,
Tigopesa, Airtel Money, Ezypesa ambalo ndilo kundi kubwa la Watanzania
wanaotumia huduma hiyo nchini.
Aawali
kodi ya bidhaa ilikuwa asilimia 10 lakini kwa hatua ya kuongezwa kwa
kodi ya ongezeko la thamani kodi itapaa na kufikia asilimia 28.
Kwa mantiki hiyo, katika kila Sh 100 kodi ni Sh 28 na katika Sh 1000 kodi ni Sh 280.
Kutokana
na hali hiyo kodi ya VAT hulipwa na mtumiaji wa mwisho ambaye anatuma
au kupokea fedha, hali ambayo itawaumiza watumiaji wa mwisho.
“Hivyo
hivyo katika miamala ya M-pesa, Tigo pesa na kadhalika, katika kila Sh
1000 itakayokatwa kwa huduma kwenye ATM kuanzia Julai 1, 2016, Sh 280
zitachukuliwa na TRA,” alisema Zitto.
Alisema
ameshangazwa na hatua ya Serikali kuongeza kodi ya VAT kwenye utalii
hali ambayo inaweza kusababisha Tanzania kupoteza watalii wengi kwa
washindani wake kwa sababu itaongeza gharama kwa watalii.
“Kama tunataka kutumia utalii kama kichocheo cha ajira ni vema kufikiria upya suala hili,” alisema.
Akizungumzia
mapendekezo ya Serikali katika Sheria ya Kodi ya VAT ili kutoza kodi
bidhaa zinazotoka Zanzibar, alisema hatua hiyo inavunja misingi
iliyowekwa na sheria ya zamani ambayo ilifanana na ile za Zanzibar.
“Ikumbukwe
kuwa Sheria ya Kodi ya VAT ya 2014 ilivunja misingi iliyowekwa ya
sheria ya zamani ambayo ilifanana na ile ya Zanzibar. Mapendekezo ya
sasa yana madhara makubwa kwa Zanzibar kwa sababu hakuna atayewekeza
Zanzibar ili kufaidika na soko la Bara.
“Biashara
nyingi zinazozalisha Zanzibar zitahamia Tanzania Bara. Mapendekezo haya
yanaweza kusababisha mgogoro kati ya pande mbili za Muungano,” alisema.
0 comments:
Post a Comment