Monday, 6 June 2016

#YALIYOJIRI>>>>MBWANA SAMATTA PAMOJA NA WASANII WA SHIWATA WAKABIDHIWA MAENEO YAO KATIKA KIJIJI CHA WASANII WILAYANI MKURANGA..FAHAMU ZAIDI HAPA.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi (katikati) akimkabidhi cheti cha umiliki wa eneo la ukubwa wa ekari tano baba yake Mbwana Samatta kwa niaba ya mwanae Mbwana Samatta wakati wa hafla ya uwagawaji maeneo kwa ajili ya wasanii na Mwanasoka huyo bora wa ndani ya Afrika Juni, 2016 Wilayani Mkuranga.
Baadhi ya nyumba katika kijiji cha Wasaanii kama zinavyoonekana katika picha Wilayani Mkuranga.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi (wa pili kulia) akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa Shirikisho la Wasaanii Tanzania (SHIWATA) Bw. Casim Taalib (kulia) pamoja na Afisa Utamaduni Wilayani Mkuranga kukagua nyumba za Wasanii 5 Juni, 2016 Wilayani Mkuranga.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi (kushoto) akisalimiana na Afisa Utamaduni Mstaafu wa Wizara hiyo Bw. Michael Kagondela pamoja na Mwenyekiti wa Shirikisho la Wasanii Tanzania (SHIWATA) Bw. Casim Taalib (katikati) mara alipowasili katika kijiji cha Mwanzega Wilayani Mkuranga kwa aajili ya hafla ya kuwagawia maeneo Wasaanii pamoja na Mwanasoka bora ndani ya Afrika Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016.
Afisa Utamaduni Wilaya ya Mkuranga, Bw. Pembe Mlekwa (kushoto) akiwa ameongozana na na wadau mbalimbali wa masuala ya sanaa na michezo pamoja na mjumbe toka Halmashauri Wilayani hapo kuelekea katika eneo la ugawaji maeneo kwa wasanii na Mwanasoka bora ndani ya Afrika, Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi (wa pili kushoto) akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa Shirikisho la Wasanii Tanzania (SHIWATA) Bw. Casim Taalib (kushoto) pamoja na Afisa Utamaduni Wilaya ya Mkuranga, Bw. Pembe Mlekwa (wa pili kulia) mara alipowasili katika kijiji cha Mwanzega Wilayani Mkuranga kwa aajili ya hafla ya kuwagawia maeneo Wasaanii pamoja na Mwanasoka bora ndani ya Afrika Bw. Mbwana Samatta 5 Juni, 2016.

0 comments:

Post a Comment