Watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi,wameuawa katika majibizano ya risasi na askari polisi mkoani Mwanza,alfajiri ya kuamkia jana jumapili katika mapango ya mlima wa Utemini yaliyopo kata ya Mkolani jijini Mwanza.
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Ahmed Msangi,amewataja majambazi waliouwa katika majibizano ya risasi usiku kucha kuwa ni Omar Francis Kitaleti mkazi wa Nyegezi Kona,said Khamis Mbuli maarufu kama fundi bomba mkazi wa bugarika na jambazi mwingine ambaye jina lake bado halijafahamika.
Amesema majambazi hayo yalikuwa yamejificha kwenye mapango ya mlima wa Utemini kabla ya askari polisi kufanikiwa kuyaua.
Jambazi
mmoja aliyeuawa ambaye hajafahamika jina lake mwenye umri kati ya miaka
20 hadi 25 alikuwa akiwashambulia polisi kwa kutumia bastola ambapo
baada ya polisi kumpiga risasi walimpekua na kumkuta akiwa na bastola
aina ya Chinese,iliyokuwa na risasi tatu ndani ya magazine,huku
majambazi wengine waliokuwepo kwenye mapango hayo wakiendelea
kujibishana kwa risasi na askari polisi.
Kamanda
Msangi ameongeza kwamba Ijumaa Juni 3,askari polisi kwa kushirikiana na
vyombo vya ulinzi na usalama,walimkamata Omar Francis Kitaleti kwa jina
maarufu kiberiti,mkazi wa Nyegezi Kijiweni ambaye alikuwa akituhumiwa
kuhusika katika matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha kwenye maduka
ya M-pesa,Tigo Pesa na Airtel money jijini Mwanza ambaye baada ya
kuhojiwa alikiri kuhusika katika matukio hayo na aliwataja wenzake
anaoshirikiana nao na mahali walipojificha.
Omary Francis Kitaleti @Kiberiti, mmoja wa majambazi aliyeuawa na wenzake kwa risasi.
Katika mapambano hayo ya risasi na askari polisi,risasi hizo ziliweza kumpata jambazi mwenzao aitwaye Omary Francis Kitaleti aliyekuwa anawaongoza askari polisi na kufariki dunia papo hapo, na risasi nyingine ilimjeruhi askari kwenye unyayo wa mguu wake wa kulia.
Amesema
polisi kwa kutumia mbinu za medani za kivita waliweza kuzingira maeneo
hayo ya mlima wa utemini hadi alfajiri ya kuamkia Jumapili Juni 5,huku
wakijibishana risasi na majambazi hao na baada ya kuona yamezidiwa nguvu
huku kukikaribia kupambazuka ndipo yalipoamua kuondoka ndani ya mapango
hayo kwa kurusha bomu moja la kutupa kwa mkono huku yakizidisha mapigo
ya risasi kwa kutumia silaha walizokuwa nazo.
Ameongeza kuwa polisi wamekamata bunduki moja aina ya SMG iliyokuwa na risasi nane na kisu kimoja.
Kamanda
Msangi amesema majambazi watatu walifanikiwa kutoroka kutoka kwenye
mapango hayo kuelekea maeneo ya Nyasaka na baada ya jambazi mmoja
kubaini kuwa askari polisi walikua wanamfuatilia alitoa bunduki na
kutaka kuwapiga askari polisi lakini polisi waliweza kumuwahi na
kumfyatulia risasi sehemu mbalimbali za mwili wake na kufariki dunia
papo hapo.
Amesema
askari polisi wamefanya upekuzi kwenye mapango ya mlima wa Utemini na
kufanikiwa kupata vitu mbalimbali vilivyoachwa na majambazi hao ambavyo
ni pamoja na risasi nne,kisu kimoja chenye damu,kofia ya kuficha uso
nyeusi moja (mask),jiko la stove,masufuria ya kupikia, unga wa
mahindi,sukari,dagaa,chakula kilichopikwa,ngoma mbalimbali,na simu tatu
za mkononi.
Askari aliyejeruhiwa amelazwa hospitali ya rufaa ya bugando na hali yake inaendelea vizuri,polisi bado wanaendelea na msako wa kuwatafuta majambazi waliofanikiwa kutoroka.
Askari aliyejeruhiwa amelazwa hospitali ya rufaa ya bugando na hali yake inaendelea vizuri,polisi bado wanaendelea na msako wa kuwatafuta majambazi waliofanikiwa kutoroka.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo alitembelea
kwenye mapango ya Utemini na kuwaomba wananchi kuendelea kutoa
ushirikiano kwa jeshi la polisi katika kuwafichua wahalifu
0 comments:
Post a Comment