KUANZIA
Julai mosi mwaka huu, serikali imepiga marufuku kwa Wizara, Taasisi,
Wakala za Serikali, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufanya
biashara na wazabuni na wafanyabiashara wengine ambao hawatumii mashine
za kielektroniki - EFDs.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema hayo jana bungeni wakati
akiwasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni
mjini Dodoma jana.
Aidha,
Dk Mpango aliwapongeza wafanyabiashara walioitikia matakwa ya Sheria ya
Usimamizi wa Kodi ambayo inamtaka kila mfanyabiashara isipokuwa wale
ambao wametangazwa rasmi na Kamishna wa Mamlaka ya Mapato kutotumia
mashine za EFD kutoa risiti kila anapouza bidhaa au huduma.
Alisema
ili kuwa na usimamizi mzuri wa fedha za serikali na kuhakikisha kwamba
zinatumika kama ilivyokusudiwa, kwa mamlaka aliyopewa chini ya Sheria ya
Fedha za Umma na kanuni zake, alitangaza kuwa malipo yote lazima
yaambatanishwe na ankara za madai au stakabadhi (tax invoice)
zilizotolewa na mashine za EFD.
“Kwa
sababu hiyo kuanzia tarehe 1 Julai 2016, ni marufuku kwa Wizara,
Taasisi, Wakala za Serikali, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa
kufanya biashara na wazabuni na wafanyabiashara wengine ambao hawatumii
mashine za kielektroniki - EFDs.
0 comments:
Post a Comment