Kumekuwa
na taarifa kuwa Yanga haikutuma majina ya wachezaji wake katika Mtandao
wa Usajili wa Kimataifa (TMS) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
limekaririwa likithibitisha hilo.
Lakini
uongozi wa Yanga, umesema taarifa hizo ni zinaonyesha wazi Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF), limepanga kuendeleza vita dhidi ya Yanga.
“Tumesikia
wanasema hatujatuma majina, nafikiri yamewasilishwa kwao zaidi ya mara
moja. Kama unakumbuka sisi tunashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho.
KATIBU MKUU WA YANGA, BARAKA
“Kila
mmoja anajua kwamba unatuma majina kwenye TMS na TFF pia Caf. Sasa vipi
yasiwepo kwao, au wanaficha makusudi ili kutuingiza kwenye matatizo kwa
makusudi.
“Inawezekana
wanafanya hivyo ili kuivuta Yanga mezaji kwa lengo la kuikomoa. Sisi
tuko tayari kupambana hadi haki yetu ipatikane.
“Nakukumbusha,
TFF inalijua sakata la Kessy na kwamba wamesema usajili wake
haujakamilika. Walijua vipi Kessy sasa yuko Yanga bila ya sisi kupeleka
jina lake katika listi ya majina pamoja na hiyo TMS.
“Wamemruhusu
Obey Chirwa pia baada ya kumuona kwenye listi ya majina yetu ya Caf
pamoja na ligi. Nashangaa TFF nayo imekuwa mshindani wa Yanga utafikiri
nayo ni klabu,” alieleza mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye amesisitiza,
hawatakubali na TFF wanapaswa kujua Yanga si klabu ya kuonewa.
TFF na Yanga zimekuwa katika mgogoro mkubwa, kila upande ukipambana na mwingine.
TFF
ilianza kuonyesha hasira zake baada ya Yanga kuwaruhusu mashabiki wa
soka kuingia bure katika mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya TP
Mazembe.
Lakini
kama haitoshi Yanga ikapitisha suala la malipo kufanyika kwa hundi
katika mechi dhidi ya Medeama, jambo ambalo lilizidi kuikera TFF, jambo
ambalo linaonyesha kuzidi kuamsha hali ya sintofahamu kati ya Yanga na
shirikisho hilo ambalo linaongozwa na Rais Jamal Malinzi na Katibu wake,
Mwesigwa Celestine, wote waliwahi kuwa makatibu wakuu wa Yanga kwa
nyakati tofauti.
0 comments:
Post a Comment