Biashara ya Bodaboda imeshamiri sana katika Jiji la Dar es Salaam lenye wakazi zaidi ya milioni nne. Hata hivyo, licha ya ukweli kwamba helmeti kupunguza kwa 69% hatari ya mwendesha pikipiki kuumia kichwa pale apatapo ajali, na kapunguza kifo kwa 42%, lakini uvaaji wa helmeti kwa madereva na abiria wao bado ni kitendawili mpaka sasa.
Kamanda wa Usalama Barabarani Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Awadhi Haji anasema wameshatoa elimu ya kutosha kwa waendesha pikipiki ili wahakikishe wanavaa kofia ngumu pamoja na abiria wao wakati wanapopanda pikipiki.
Na kwa Watakaokaidi agizo hilo watakamatwa wao na abiria wao na kufikishwa mahakamani. Ambako wanaweza kutozwa faini inayoanzia Sh 300,000 au kufungwa jela kati ya miezi sita au mwaka mmoja kutokana na sheria ya Sumatra.
Polisi wameamua kufanya hivyo kutokana na faini ya Sh 30,000 chini ya sheria ya usalama barabarani kutowaogopesha madereva wengi wa pikipiki. Ndiyo maana sasa uamuzi ni kuwapeleka mahakamani moja kwa moja.
0 comments:
Post a Comment