Home »
Michezo
» #MICHEZO>>>>PAWASA- OMOG ANAKOSEA KUWACHEZESHA AJIB NA MAVUGO.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Beki wa zamani wa Simba na Taifa Stars,
Boniface Pawasa, ameangalia mfumo unaotumiwa na Kocha Mkuu wa Simba,
Joseph Omog, kisha akasema kama kweli anataka wafunge mabao mengi, basi
ni lazima aubadilishe.
Pawasa amekosoa mfumo huo wa Omog wa
kuwapanga pamoja washambuliaji Laudit Mavugo na Ibrahim Ajib kwa wakati
mmoja huku akisema washambuliaji hao wanacheza soka la kufanana.
“Ukiangalia uchezaji wa Mavugo ni kama
namba kumi, pia Ajib anacheza kama hivyo, yaani wote wakiwa katika
kikosi cha kwanza utaona anakosekana mshambuliaji wa mwisho ambaye muda
wote anatakiwa kuwa kwenye eneo la hatari la wapinzani.
“Kwa mfumo anaoutumia Omog, hana budi kuwachezesha Ajib na yule
Muivory Coast (Frederic Blagnon) au Mavugo na huyo jamaa (Blagnon) kwani
yeye nimemuona ndiye anaweza kucheza kama mshambuliaji wa mwisho
tofauti na hao wengine.
“Kama Omog akiendelea kuwatumia zaidi Ajib na Mavugo kwa pamoja, basi
watakuwa na kazi kubwa ya kufanya kwenye kusaka ushindi, wanaweza
kushinda lakini si kirahisi,” alisema Pawasa.
0 comments:
Post a Comment