Home »
Habari Moto
» #YALIYOJIRI>>>WAGONJWA KUTOKA NNJE YA NCHI WAJA NCHINI KUTIBIWA MOYO.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Matunda ya taasisi ya moyo ya JAKAYA
KIKWETE yanazidi kuonekana baada ya wagonjwa mbalimbali kutoka nje ya
nchi kufika katika taasisi hiyo kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Wakizungumza katika tasisi hiyo baadhi
ya wagonjwa wamesema taasisi hiyo inatoa huduma bora na zenye kuridhisha
sawa na hospitali nyingine nje ya AFRIKA.
Katika siku ya pili ya upasuaji kwa
watoto zaidi ya 50 wenye matatizo ya moyo kwa ushirikiano wa madaktari
toka MAREKANI na TANZANIA, watoto watano wanatoka katika nchi za Jamhuri
ya Kidemokrasi ya Kongo na UGANDA kama anavyoelezea mkurugenzi mtendaji
wa taasisi hiyo Prof: MOHAMED JANABI.
Kiongozi wa watoto waliotoka nchini UGANDA JOHN FRANCIS ameeleza kuridhishwa kwake na huduma walizopata watoto aliokuja nao.
Baadhi ya mashirika yameanza kujitolea
kugharamia za matibabu kwa watoto wenye matatizo ya moyo likiwemo
shirika la BAPPS CHARITIES TANZANIA ambao wametoa shilingi Milioni 220
kugharamia matibabu kwa watoto 100.
Tayari watoto SITA wamefanyiwa
upasuaji mkubwa katika siku mbili tangu kuanza kwa zoezi la upasuaji
litakalodumu hadi SEPTEMBA 19.
0 comments:
Post a Comment