Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya dawa za kulevya inayomkabili msanii Agnes Gerald Waya maarufu kama Masogange baada ya kutohudhuria kesi hiyo mahakamani.
Kesi
hiyo ambayo imetajwa kwa mara ya kwanza mbele ya hakimu mkazi wa Kisutu
Wilbard Mashauri wakili wa serikali Adolf Mkini amesema kuwa mshtakiwa
anakabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin
na Oxazepham.
Ameeleza
kuwa mshitakiwa anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14, 2017 katika
maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam alitumia dawa za
kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine) na kuwa kati ya Februari 7 na
14, 2017 alitumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.
Mshitakiwa
anadaiwa kufanya makosa hayo chini ya kifungu cha 18 (a) cha sheria ya
kupambana na dawa za kulevya namba 5 ya mwaka 2015 na kuwa uopelelezi wa
kesi hiyo bado haujakamilika licha ya mshtakiwa kutokuwepo mahakamani
hapo.
Hata hivyo wakili wa Masogange, Nictogen Itege aliwasilisha udhuru mahakamani hapo juu ya mteja wake kutokuwepo.
Licha
ya maelezo hayo Hakimu Mashauri alimtaka mshtakiwa kuheshimu masharti
ya mahakama na kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 20, mwaka huu
mshitakiwa yupo nje kwa dhamana.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment