Na: LilianLundo – MAELEZO
Serikali
imefuta usajili wa vibali vya uzalishaji na Uingizaji wa aina 20 ya
pombe kali za viroba zilizokuwa zimesajiliwa na Mamlaka ya Chakula na
Dawa (TFDA).
Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
ameyasema hayo leo, Jijini Dar es Salaam kuhusu usitishaji wa uzalishaji
na uingizaji, uuzaji na matumizi ya pombe zilizofungwa katika mifuko ya
plastiki (Viroba).
“Tumefuta
usajili wa vibali vya uzalishaji na uingizaji kutoka nje, usambazaji,
uuzaji na matumizi ya pombe kali zilizofungashwa katika mifuko ya
plastiki (viroba) chini ya ujazo wa milimita 200,” alifafanua Ummy Mwalimu.
Aliendelea
kwa kusema kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa tamko la Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa alilotoa Februari 02, 2017 la kusitisha uzalishaji,
uingizaji, usambazaji, uuzaji na matumizi ya pombe hiyo kali kuanzia
Machi 01, 2017.
Ummy
amesema kuwa usitishaji huo unazingatia kanuni za kukataza uzalishaji,
uingizaji na matumizi ya vifungashio vya plastiki kufungashia pombe kali
za mwaka 2017 (The Environmental Management (Prohibition of
Manufacturing, Important and Use of Plastic Sachets for Packakging
Distilled and other alcoholic beverages) Regulations 2017) imekatazwa
kutumia vifungashio vya plastiki kufungashia pombe kali. Badala yake
wazalishaji watapaswa kufungasha pombe kali hizo katika chupa zenye
ujazo usiopungua mililita 200.
Aidha
amesema kuwa uamuzi wa kupiga marufuku matumizi ya pombe za aina hiyo
unatokana na athari mbalimbali ikiwa ni pamoja na za kiafya na kijamii.
Matumizi mabaya ya pombe hizo yamesababisha ajali nyingi, vifo, ulemavu
na mzigo mkubwa kwa Serikali wa kutoa huduma kwa wahanga wa pombe hizo
na ongezeko la makosa ya jinai.
Ummy amesema kwamba Viroba vilivyokamatwa na kuzuiwa vinasubiri maelekezo kutoka ofisi ya Waziri Mkuu namna ya kuviteketeza.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment