WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha sukari cha Kampuni ya
Alteo ya Nchini Mauritius chenye uwezo wa kukamua tani 400 za miwa kwa
saa na kuzalisha tani 170,000 za sukari kwa mwaka.
Kampuni
ya Alteo inamiliki kiwanda cha sukari cha TPC mkoani Kilimanjaro kwa
ubia na Serikali ya Tanzania na kinazalisha tani 110,000 kwa mwaka.
Waziri
Mkuu ametembelea kiwanda hicho leo (Jumanne, Machi 21, 2017) na
kujionea namna wanavyozalisha sukari kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
Aidha, Waziri Mkuu amefanya mazungumzo na uongozi wa kiwanda hicho na kuwashawishi waongeze maeneo ya uwekezaji nchini.
“Tekonolojia
wanayoitumia katika uendeshaji wa kiwanda chao ni nzuri hivyo
tumewashawishi waje kuongeza maeneo ya uzalishaji wa sukari nchini ili
tuweze kukidhi mahitaji,” amesema.
Waziri
Mkuu amesema Tanzania kuna viwanda vitano vya sukari ambavyo ni Mtibwa,
Mahonda (Zanzibar), TPC, Kilombero na Kagera vinavyozalisha tani
320,000 kwa mwaka huku mahitaji ni tani 420,000.
Kwa
upande wake Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohammed amesema Zanzibar kuna kiwanda
kimoja cha sukari ambacho uzalishaji wake haukidhi mahitaji kutokana na
uhaba wa malighafi.
Kutokana
na hali hiyo, Dkt. Khalid ameikaribisha kampuni ya Alteo kwenda
Zanzibar kushirikiana na Serikali katika uwekezaji hususani kwenye
viwanda vya sukari. Naye Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Patrick de
Labauve amesema wamekubali kuongeza maeneo ya uwekezani wa mashamba ya
miwa nchini.
Pia
ameomba Serikali iwapatie fursa ya uwekezaji katika sekta ya utalii
mkoani Kilimanjaro. “ Kuna vivutio vingi vya utalii ukiwemo mlima
Kilimanjaro,”.
Akizungumzia kuhusu ajira amesema kiwanda cha TPC kimeajiri wafanyakazi 3,000 wakiwemo 1,900 wa kudumu.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, MACHI 21, 2017.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment