Thursday 22 December 2016

Azikwa kaburi moja na Kondoo, Iringa.Fahamu zaidi hapa.

MAMIA  ya  wakazi  wa kijiji  cha  Mbigili na  mji  wa Ilula  katika  wilaya ya  Kilolo, mkoani Iringa jana walifurika katika mazishi  ya aina  yake  yaliyofanyika katika kitongoji  cha Mkawaganga  kijiji  cha Mbigili  wilaya ya  Kilolo mkoani Iringa  kushuhudia mazishi ya  kihistoria baada ya mzee mmoja aliyefariki  dunia ghafla  kuzikwa kaburi  moja na kondoo pamoja na kuku mweusi.

Tukio hilo  limetokea wakati  wa mazishi ya mzee Andrea Ngaga (90) mkazi wa kitongoji  cha Mkawaganga  aliyekuwa  akijishughulisha na kazi  za uganga  wa kienyeji kijijini  hapo enzi  za  uhai  wake .

Baadhi ya  wananchi  waliofika katika mazishi  hayo  walisema  kuwa  walilazimika  kusitisha shughuli  zao za  shamba na biashara na  kufika  kushuhudia  mazishi hayo ambayo ni mara ya kwanza  kufanyika katika  kijiji  hicho  alisema  John  Mfaligoha  kuwa  kabla ya  kifo marehemu  huyo  alipata  kuwaeleza  aina ya mazishi yake  yatakavyokuwa .

Hivyo alisema  wananchi waliowengi walifika  kutaka  kushuhudia tukio  hilo la mazishi  na  ndio  sababu  iliyopelekea  wananchi kusukumana msibani  wakati wa mazishi  kwa  kila mmoja kutaka  kushuhudia  tukio  hilo la kihistoria katika kijiji hicho.



Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

0 comments:

Post a Comment