Thursday 22 December 2016

Wakulima wakutwa na kilo 5,000 za bangi.Fahamu zaidi hapa.

POLISI mkoani Morogoro wakishirikiana na kikosi kazi cha taifa cha kupambana na dawa za kulevya wamekamata tani tano za bangi, mbegu zake zaidi ya kilo 300 na nyara za serikali yakiwemo magamba 42 ya mnyama adimu kakakuona.

Watu wawili wamekamatwa kuhusu sakata hilo. Watuhumiwa hao wamekamatwa katika operesheni maalumu kuanzia Desemba 16 hadi 19, mwaka huu katika wilaya ya Kilosa na Mvomero.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, (SACP), Ulrich Matei, amesema jana kuwa, Polisi wa mkoa, na timu maalumu ya kuratibu na kudhibiti dawa za kulevya kitaifa ikiongozwa na SACP, Mihayo Msikhela wamewakamata watuhumiwa Ally Rashid Abdallah Manji (36) na Julius Keneth (40). Amesema, Manji alikamatwa Desemba 19, mwaka huu majira ya saa tatu asubuhi maeneo ya Kipara, kijiji cha Msengele, Kata ya Doma, Tarafa ya Mlali, wilaya ya Mvomero kwa kushirikiana na kikosi cha kudhibiti dawa za kulevya taifa.

Walipompekua mtuhumiwa huyo mbaye ni mkulima na mkazi wa Doma alikutwa akiwa na bangi viroba 11 vyenye uzito wa kilo 800 ambapo vitano vilikuwa na mbegu na vingine sita vikiwa na bangi yenyewe.

Kamanda Matei alisema katika upekuzi wa kibanda hicho mtuhumiwa huyo pia alikutwa na nyara za serikali bila kuwa na vibali vyovyote.

Nyara hizo ni ngozi ya fungo na magamba 42 ya kakakuona.

Mtuhumiwa huyo alikutwa akimiliki shamba la bangi lenye ukubwa wa ekari 20 na walilitekeleza na moto.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

0 comments:

Post a Comment