Wednesday 28 December 2016

Yafahamu matunda ambayo hupunguza maumivu makali wakati wa hedhi.Fahamu zaidi hapa.

Mzunguko wa hedhi ni mzunguko wa kila mwezi ambao mwanamke huupata, hali ambayo huleta kutokwa na damu ukeni kutokana na mimba kutotungwa. Kwa hali ya kawaida hedhi ya kwanza hutokea katika umri wa miaka 12 -13 na kuendelea.

Hedhi hutokea pale ambapo tishu za ukuta wa mji wa mimba zinapobomoka na kutoka kama damu ukeni.
Hata hivyo, kumekuwepo na wanawake kadhaa ambao wamekuwa wakijuta kuingia kwenye mzunguko wao kutokana na kuambatana na maumivu makali na kupelekea hata kushindwa kufanya shughuli zao za kila siku.

Leo ninayo orodha ya matunda ambayo yakitumika huweza kupunguza maumivu wakati wa kipindi hicho.
Matunda hayo ni haya yafuatayo:-
Nanasi.
Hili ni miongoni kati ya matunda yenye uwezo wa kupiunguza maumivu hayo yatokanayo na mzunguko (hedhi) hii ni kutokana na tunda hili kuwa na virutubisho vyenye uwezo wa kuifanya misuli ya sehemu za siri za kike kuwa huru (kurelax) na hivyo kupunguza uwezekano wa maumivu makali.
Ndizi
Kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri wa umuhimu wa matunda nadhani utakuwa umewahi kusikia kuhusu umuhimu wa ndizi hata kwa wanamichezo na imekuwa ikiwasaidia kurekebisha misuli na kuondoa tatizo la kukaza kwa misuli mara baada ya mazoezi, hivyo basi tunda hili pia huweza kuwasaidia wanawake ambao wanapatwa na maumivu makali wakati wa hedhi na kupunguza au kuondoa hali hiyo kabisa.
 Pamoja na kukueleza kuwa matunda hayo huweza kupunguza maumivu wakati wa mzunguko lakini ni vyema kuzingatia kuwa matunda hayo yanapaswa kuliwa angalau siku mbili au moja kabla ya kuingia kwenye mzunguko wako ili kupata matokeo mazuri zaidi.

Pia unashauriwa kunywa maji ya kutosha kipindi cha mzunguko kwani nayo huwa na nafasi kubwa ya kusaidia kupunguza kiwango cha maumivu hayo.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com
Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

0 comments:

Post a Comment