Wednesday 28 December 2016

HUU NDO MTAA UNAO ONGOZA KWA USHOGA DAR.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Wakazi wa mtaa wa Keko Machungwa kata ya Miburani wilaya Temeke jijini Dar es salaam wamedai mtaa wao unakabiliwa na changamoto ya ongezeko kubwa la watoto wanaoingia kwenye ushoga hali ambayo ina hatarisha malezi ya watoto wengine ambao wanaishi katika mtaa huo.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Keko Machungwa Mr Mashaka (katikati)

Hayo yameibuliwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Keko Machungwa Mr Mashaka Ramadhani baada ya kutembelewa katika mtaa wake na wanafunzi ambao wanapambania haki za watoto kutoka chuo kikuu cha Dar Es Salaam University College of Education (DUCE) kwa ajili ya kutoa elimu ya haki za watoto kwa baadhi ya watoto wa mtaa huo pamoja na wazazi ndipo changamoto hiyo ikaibuka.
 
Akiongea mbele ya waandishi waliojitokeza katika mafunzo hayo, Mwenyekiti huyo alidai mtoto wengi wanajiingiza katika matendo mabaya kutokana na malezi mabaya ya mawazi pamoja na mtaa huo kujengwa kiholela.
 
“Katika mtaa wetu kumekuwa na changamoto nyingi lakini kwa upande wa watoto kumekuwa na wimbi la watoto kuingia kwenye ushoga kama ulivyosikia,” alisema Mashaka. “Kwa hiyo ujio wa watu kama hawa katika mtaa wetu unaweza kusaidia kutoa elimu kwa wazazi juu ya malezi bora, kufuatilia mwenendo ya watoto wetu wakiwa shuleni na nyumbani pamoja na kuangalia marafiki ambao anatembea nao,”
Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar Es Salaam University College of Education (DUCE) Emijidius Cornel ambaye ni mmoja kati ya wanafunzi walioandaa tukio hilo(kushoto) akiwa na Diwani wa kata hiyo, Juma R. Mkenga

Pia mwenyekiti huyo alidai mtaa huo mwenye wakazi 12,400 unakabiliwa na ujenzi holela kutokana na viwanja na eneo hilo kutopimwa hali ambayo imesababisha mtaa huo kuwa navichochoro vingi.
“Kuna changamoto nyingi kama nilivyosema lakini pia huu mtaa viwanja vyake havijapimwa, kwa hiyo kumekuwa na mbanano wa nyumba sana na wakazi ni wengi,”
 
Kwa upande wa Diwani wa kata ya hiyo Juma R. Mkenga ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa mtaa huo kabla ya kuwa Diwani, alikiri kuwepo kwa watoto wa namna hiyo ambapo pia aliwataka wazazi wa mtaa huo kuwa makini na watoto wao ili kuwaepusha kuingia kwenye janga hilo.
 
Mmoja kati ya wakazi wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina la Mama Happy, alidai watoto wao wapo kwenye mazingira hatarishi kutokana na watoto wengi wa mtaa huo kuingia kwenye janga hilo.
 
“Hapa watoto ambao ni mashoga wapo wengi sana, yaani wapo wengi mpaka wengine tunawajua kwa majina kabisa na idadi ni kubwa, tena wengine hawajifichi kabisa, wanaeleza,” alisema mama huyo.
 
Mama huyo mwenye watoto wawili alidai watoto wa shule za msingi wenye umri kuanzia miaka 10 na kuendelea ndio waathirika wakuu wa janga hilo huku akiitaka serikali pamoja na wazazi kulifuatilia suala hilo kwa ukaribu zaidi.
 
“Suala hili kwa upande wangu naona lina sababishwa na wazazi kutowafuatilia watoto wao, mzazi mtoto toka anaanza la kwanza hadi la saba hajawahi kwenda shule wala kujua mtoto wake anafanya nini shule. 
 
Kwa hiyo watoto wengi wanadanganya wapo shule kumbe wapo vichakani wanafanya vitu vyao,” alisema Mama huyo.
 
Aliongeza “Pia yaha mambo yamesababishwa na vikundi, wengine tamaa za maisha kutoka mashuleni, uvutaji wa bangi pamoja na uhuru mwingi wanaopewa na wazazi. Mimi na mtoto mmoja wa kike na mwingine wakiume lakini ukifika muda wa jioni tu nahakikisha mtoto wangu wapo ndani kwa sababu hii hali sio nzuri na inatisha, nimekaa sehemu nyingi lakini mtaa huu kiboko,”
 
Mzazi huyo ameiomba serikali ya mtaa pamoja na serikali ya mkoa wa Dar es salaam kufuatilia sakata hilo kwa makini ili kujaribu kulidhiti haraka iwezekanavyo.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

0 comments:

Post a Comment