Wednesday 28 December 2016

#BREAKING NEWS>>>Dhamana ya Mbunge Lema yakwaa kisiki mahakamani, arejeshwa rumande.Fahamu zaidi hapa.

Mbunge Godbless Lema amerejeshwa tena rumande leo baada ya rufaa yake ya kupinga kunyimwa dhamana kushindikana kusikilizwa kama ilivyokuwa imepangwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo.

Rufaa hiyo ya Lema iliyokuwa umepangwa kusikilizwa leo imeshindikana baada ya upande wa Jamhuri kukata rufaa kupinga kuongezwa muda wa kuwasilisha notisi ya rufaa.

Upande wa mtuhumiwa uliongezea muda wa kuwasilisha notisi ya kukata rufaa kupinga kunyimwa dhamana baada ya kushindwa kufanya hivyo katika muda uliokuwa umepangwa awali.

Mbunge Godbless Lema ambaye alikamatwa Novemba 2 mwaka huu mjini Dodoma amerejeshwa rumande katika gereza la Kisongo jijini Arusha.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

0 comments:

Post a Comment