Saturday 24 December 2016

MENEJA BABU TALE:CHIDI BENZ NI SIKIO LA KUFA.Fahamu zaidi hapa.

Leo muda mchache uliopita team nzima ya WCB Wasafi na team ya XXL walikuwa pande za Mlimani City jijini Dar es Salaam kwenye tukio zima la kuuza tiketi kwaajili ya show ya kesho pande za Jangwani Sea Breez kwenye Wasafi Beach Party.
 

Wakali hao waliweza kukutana na mashabiki zao ana kwa ana na kuruhusu maswali mawili matatu kutoka kwa mashabiki. Mmoja kati ya watu ambao walipokea maswali kutoka kwa mashabiki ni pamoja na meneja wa Diamond Platnumz mtu mzima Babu Tale.
 
Swali ambalo aliulizwa meneja huyo ilikuwa ni kuhusu rapper Chidi Benzi ambaye tetesi za kitaa zinasema amerudi tena kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya ikiwa hapo awali meneja huyo allisikika kujitolea kumsaidia rapper huyo
“Chidi Benz nimemsaidia kwasababu mimi ni mtoto wa kiume na nimezaa watoto wa kiume, lakini wanasemaga sikio la kufa halisikii dawa. Mimi nimemsaidia lakini ikafika wakati nikashindwa kwasababu niliona mtu ndio vile vile hajaacha ikanibidi nikae pembeni.”
 
Hayo ni baadhi tu kati ya mengi ambayo Babu Tale amefunguka kuhusiana na Chidi Benz. Unaweza kumsikiliza yeye mwenyewe akifunguka mwanzo hadi mwisho kwa kuplay hii video hapa chini.



Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

0 comments:

Post a Comment