Kauli mbalimbali zinazoendelea kutolewa na Rais John Magufuli, zimezua mjadala miongoni mwa wasomi nchini.
Kwa
mfano, wanasema kauli ya kukosoa udahili wa wanafunzi katika Chuo Kikuu
cha Dodoma (Udom) na ile ya kuelekeza hatua za kuchukua dhidi ya watu
wanaotumia kimakosa barabara za Mabasi Yaendayo Haraka (Udart),
inaashiria kuna tatizo kubwa la utendaji serikalini.
Walisema
ni jambo lisiloingia akilini, wanafunzi wadahiliwe na kuanza masomo
kisha baadaye wafukuzwe kwa maelezo kuwa Serikali haiwezi kulipia ada
wanafunzi ‘vilaza’.
Akizungumzia kauli hizo jana, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dk James Jesse alisema hakuna sheria za usalama barabarani zinazotamka mtu akifanya kosa gari lake litolewe magurudumu.
Juzi
wakati akiweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa maktaba ya kisasa
ya UDSM, Rais Magufuli alisema mpango maalumu uliopitishwa na Serikali
ya Awamu ya Nne wa wanafunzi kusoma diploma ya ualimu Udom, unajumuisha
waliofeli.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Hamad Salim alihoji: “Rais
amesema wanafunzi waliopo Udom ni vilaza ila waziri wa elimu (Profesa
Joyce Ndalichako) alisema wanafunzi wanaosoma mafunzo hayo hakuna
aliyepata daraja la nne. Sasa hapo nani mkweli.”
“Kupishana huku kwa kauli kunatupa mashaka na utendaji kazi wa baadhi ya viongozi serikalini."
Hamad alisema suala kama hilo lilipaswa kutolewa ufafanuzi na waziri husika na si Rais.
Alisema umefikia wakati wa kiongozi huyo mkuu wa nchi kubaini changamoto na kutoa maelekezo na si kuzungumzia kila kitu.
0 comments:
Post a Comment