Home »
Makala
» KINACHOPELEKEA KUTOKUPEVUKA KWA MFUMO WA UZAZI.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Hali hii hutokana na viungo vya
uzalishaji wa vichocheo vya uimarishaji uzazi kwa mwanamke na mwanaume
kutofanya kazi. Viungo au Glandi hizi ni korodani kwa mwanaume na ovari
kwa mwanamke.
Tatizo hili linaweza kuwa linatokea
tangu kuzaliwa au linatokea katika mfumo mzima wa mwili. Kwa tatizo la
kuzaliwa nalo, korodani au vifuko vya mayai huwa havifanyi kazi ya
kuzalisha vichocheo au homoni zinazohitajika ambapo kwa korodani
huzalisha homoni za kiume na ovari huzalisha homoni za kike.
Vyanzo vya matatizo ni kama vile:-
– Matatizo katika mfumo wa kinga mwilini.
– Matatizo katika mfumo wa vinasaba.
– Matatizo ya ini na figo.
DALILI ZA TATIZO
Dalili kwa mtoto wa kike ambaye
hajavunja ungo, utamwona bado ni mtoto yaani habadiliki yupo vilevile
tangu alipokuwa na umri wa miaka kumi hadi anafikisha ishirini, matiti
hayakui, urefu haongezeki. Kama tatizo likitokea baada ya kuvunja ungo
huhisi joto muda wote hata kama kuna baridi, nywele sehemu za siri na
makwapani hupuputika zenyewe, hupoteza hamu ya tendo la ndoa kabisa na
haendelei tena kupata siku zake na kufunga hata zaidi ya mwaka.
Ukiwa na dalili hizo, muone daktari kwa ushauri zaidi.
0 comments:
Post a Comment