Kiungo wa zamani wa Manchester United, Paul Scholes amewakosoa mabeki wa
timu hiyo, Daley Blind na Antonio Valencia kwa jili walivyocheza katika
mchezo wa Manchester derby dhidi ya Manchester City.
Scholes
amenukuliwa akisema: “Blind ni zuri akichea kama kiungo mkabaji na siyo
beki wa kati, japokuwa hivi karibuni amekuwa akielewana na Eric Bailly.
“Nashindwa kuelewa kwa nini Chris Smalling hachezi.
“Ningependelea kumuona Smalling akicheza pamoja na Bailly.”
Kuhusu Valencia, mkongwe huyo alisema: “Valencia siyo beki wa kulia na hatakuwa kamwe, Matteo Darmian hajapata kasi ya kuendana na ligi na ninachojiuliza kama Timothy Fosu-Mensah anaweza kuanza katika kikosi cha kwanza au la, nafikiri kuan tatizo hapo.”
0 comments:
Post a Comment