Klabu
ya Manchester United imetangaza kuwa imeingiza mapato ya pauni milioni
515.3 katika msimu wa mwaka mmoja uliopita uliomalizika Juni 30, 2016.
Kutokana
na kiwango hicho, klabu hiyo imesema kuwa imepata faida ya pauni 68 na
kuwa klabu ya kwanza ya Uingereza kuingiza pato la zaidi ya pauni nusu
pauni ndani ya mwaka moja na pia imekuwa ya pili kwa kuingiza fedha
nyingi nyuma ya Barcelona ya Hispania kwa ujumla.
Licha ya kushindwa kufuzu kucheza katika Uefa Champions League, bado klabu hiyo imeendelea kuingiza mapato mengi kupitia malipo ya wadhamini yakiwemo yale ya runinga.
Mtendaji
Mkuu wa Man United, Ed Woodward amesema kuwa: "Kuteuliwa kwa Jose
Mourinho ni moja ya njia zetu za kutufanya kuwa bora na kurejea kwenye
ubora wetu, tupo katika mchamkato wa kuandika ukurasa mpya wa historia
ya soka.”
Pamoja na hivyo, United ambayo ipo katika mkataba wa pauni milioni 750 ndani ya miaka 10 na kampuni ya adidas katika masuala ya jezi inatajwa kuwa na deni la pauni milioni 260.9.
Takwimu zinaonyesha kumfukuza kazi Louis van Gaal na wasaidizi wake kulisababisha klabu hiyo kupoteza pauni milioni 8.4 kama fidia.

0 comments:
Post a Comment