YAWEZEKANA ikawa ni moja ya sababu ya mvua kuchelewa kunyesha mkoani Iringa tofauti na ilivyozoeleka miaka mingine ni kutokana na laana kama hizi baada ya kikosi maaalum kinachoongozwa mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwa kushirikiana na OFM kufanikiw kumkamata kijana Emmanuel Mkiwa (19) kwa tuhuma za kumbaka mara kwa
mara mdogo wake wa miaka (4)
Afisa maendeleo ya jamii Manispaa ya Iringa Josephina Mwaipopo akiwa na mtoto aliyebakwa
Imedaiwa kuwa kijana huyo ambae
ni mwenyeji wa mtaa wa Omary Matrekta kata ya Mtwivila katika
Manispaa ya Iringa alikuwa akiishi nyumba moja na babake pamoja na
wadogo zake watatu wawili wa kiume na mmoja ni mtoto huyo wa
miaka 4 ambaye alitelekezwa na mamake mzazi kutokana na mambo ya
kifamilia kati yake baba wa mtoto .
Mashuhuda wa tukio hilo
lililotokea January 16 majira ya saa 2 usiku walimweleza mwandishi
wa OFM Iringa kuwa kijana huyo mara kwa mara alikuwa akimbaka
mdogo wake huyo ambae baba mmoja na mama tofauti kabla ya mtoto
huyo kuwaeleza majirani kuwa kakake huyo amekuwa akimkandamiza na
kijiti sehemu zake za siri (Akimbaka)
Kutokana na maelezo ya mtoto
huyo ndipo taarifa za raia wema hao zilipofikishwa kwa mkuu wa
wilaya na OFM na kuamua kufika katika eneo la tukio na kufanikiwa
kumkamata kijana huyo na baba mzazi wa watoto hao Shukuru Mkiwa
kwa malezi mabaya ya watoto.
Akizungumza baada ya kukamatwa
kwa kijana huyo mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela
pamoja na kuwashukuru raia wema kwa kufikisha taaarifa ya
kunyanyaswa kwa mtoto huyo bado alitoa wito kwa wananchi wengine
ambao wanataarifa za kunyanyaswa kwa mtoto yeyote katika wilaya
ya Iringa kutoa taarifa ili wahusika wakamatwe na kufikishwa
katika vyombo vya sheria.
Kasesela
alisema kuwa uchunguzi uliofanywa baada ya vipimo katika Hospitali
ya Rufaa ya mkoa wa Iringa umeonyesha mtoto huyo kashaondolewa
usichana wake na hivyo kulazimika kulazwa kwa matibabu katika
Hospitali hiyo huku akiahidi kumsaidia mtoto huyo kumsomesha .
Alisema
kuwa yawezekana moja ya sababu ya mvua kuchelewa kunyesha katika
mkoa wa Iringa ni pamoja na matukio ya kinyama kama haya ya
ubakaji watoto na kuwa hatakubali kuona mbakaji anaendelea kuishi
uraiani wilaya ya Iringa kwani tayari mkuu wa mkoa wa Iringa Amina
Masenza kupitia kikao cha makati ya ushauri ya mkoa (RCC) aliagiza
wabakaji wote wasakwe kwa udi na uvumba na yeye ameanza
kutekeleza agizo hilo.
kutekeleza agizo hilo.
Japo alisema alishangazwa na
hatua ya baba mzazi wa kijana huyo kumficha mbakaji ndani na
kudanganya kuwa hayupo wakati kijana wake alikuwepo ndani hivyo
mzazi huyo kukamatwa pamoja na kijana wake yeye kwa kosa la
kumchifa mharifu na kijana wake kwa kosa la ubakaji .
“Hiki ni kikosi kamili ambacho kitaendelea kuendesha misako mbali mbali kwa kushirikiana na oparesheni Fichua Maovu (OFM)
ya Global Publishers hivyo kwa yeyote anayejua wapi mtoto
anafanyiwa vitendo vya kikatili piga simu hii mwandishi wa OFM Iringa
0754 026 299 tutakufikia ulipo na
kuchukua hatua”
kuchukua hatua”
Jeshi
la polisi mkoa wa Iringa kupitia kwa kamanda wa polisi mkoa
(RPC) Julius Mjengi limethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na
kuwa baada ya upalelezi atafikishwa mahakamani huku likiwataka
wananchi kuendelea kufichua waharifu zaidi
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment