Mahakama
ya Mkoa wa Lindi, imemuhukumu kwenda jela miezi nane, Suleiman Mathew
ambaye alikuwa mpinzani wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Nape Nnauye katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 katika Jimbo la
Mtama.
Mathew
ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Lindi na kiongozi mwenzake
wa kata wamehukumiwa kwenda jela baada ya kupatikana na hatia ya kufanya
mkusanyiko bila ya kibali.
Hukumu hiyo ilitolewa jana katika Mahakama ya Mkoa wa Lindi, mbele ya Hakimu Mkazi Godfrey Mhina.
Mahakama
imefikia uamuzi huo baada ya kusikiliza mashahidi sita wa upande wa
mashtaka na kujiridhisha kuwa ushahidi wao umethibitika bila kuacha
shaka.
Waliotiwa
hatiani na kupewa adhabu hiyo ni Mwenyekiti Chadema mkoani Lindi,
Selemani Methew pamoja na Katibu wa Tawi la Kata ya Nyangamala, Ismail
Kupilila.
Akisoma
hukumu hiyo Hakimu Mhina alisema, upande wa mashtaka ukiongozwa na
Wakili wa Serikali Juma Maige uliwafikisha mahakamani hapo mashahidi
sita.
Alisema
kutokana na ushahidi ulitolewa na mashahidi hao, mahakama imeona upande
wa mashtaka umeweza kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa hao bila
kuacha shaka yoyote na kuwatia hatiani.
Baada ya kuwatia hatiani mahakama iliwapa nafasi washtakiwa ili waweze kujitetea ambapo waliomba wapunguziwe adhabu.
Akiwasilisha
hoja za upande wa utetezi Wakili wa washtakiwa hao, Deusdet Kamalamo
aliiomba mahakama isiwape adhabu kali kwa madai kwamba wanafamilia
inawategemea, hivyo iwapo watapewa adhabu kubwa kutaifanya ikose huduma
zao.
Baada
ya utetezi huo, Wakili wa Serikali Juma Maige aliiomba mahakama hiyo
iwape washtakiwa hao adhabu kwa mujibu wa sheria inavyoelekeza ili iwe
fundisho kwao na wengine.
Hakimu
Mhina akitoa adhabu katika kesi hiyo namba 36/2016, chini ya kifungu
cha 74 (1) na 75 cha kanuni ya adhabu sura ya 16, alisema mahakama
inawapa adhabu, kila mshtakiwa atatumikia kifungo cha miezi minane
gerezani na kusema nafasi ipo wazi ya kukata rufaa iwapo wataona
hawakuridhishwa na hukumu hiyo.
Baada
ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Mathew alisikika akiguna na baadae aliketi
sakafuni, huku katibu wake wa tawi, Ismail ambaye alionekana kuchoka
kutokana na hukumu hiyo akiwa amelowa kwa jasho.
Mahakama
hiyo pia iliwaachia huru washtakiwa wanne ambao ni wanachama waliokuwa
wameshtakiwa pamoja na viongozi hao, baada ya ushahidi uliokuwa
umetolewa na upande wa mashtaka kutokuwa na mashiko ya kuishawishi
mahakama kuwatia hatiani.
Washtakiwa
hao ni Bashiru Rashid, Hassani Mchihima, Abdallah Masikini na Mohamedi
Makolela ambao wote ni wakazi na wakulima wa Kata ya Nyangamala.
Awali
washtakiwa hao walidaiwa kutenda makosa hayo Aprili 3, mwaka jana,
maeneo ya Kata ya Nyangamala, mkoa Lindi, washtakiwa walifanya
mkusanyiko usio halali.
Akizungumza
nje ya mahakama hiyo, Wakili wa upande wa utetezi, Deusde Kamalamo
alisema wanajiandaa kukata rufaa kupinga uamuzi uliotolewa na mahakama
hiyo.
“Tutakata rufaa kupinga uamuzi huu, leo naandaa barua ya kuomba nakala ya hukumu ili tuanze kuandaa rufaa ya wateja wangu,” alisema Wakili Kamalamo.
Katika
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Methew alikuwa akipambana na Nape ndani ya
CCM lakini alishindwa kufurukuta katika kura za maoni na baadae
alijiengua na kujiunga na Chadema na kuwa mgombea ubunge kupitia chama
hicho.
Katika
hatua nyingine jana Diwani wa Kata ya Kyangasaga, wilayani Rorya,
Christopher Kichinda maarufu ‘Protocol’ amehukumiwa kwenda jela miaka
mitano.
Akizungumzia
hukumu hiyo Katibu wa Chadema Mkoa wa Mara, Chacha Heche, alisema
diwani huyo alikuwa anakabiliwa na kesi ya Katiba iliyokuwa inamkabili
kuwa alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya lakini
alijitoa ambapo mahakama ilimtia hatiani kwa makosa yaliyokuwa
yanamkabili.
“Ni kilio kingine kwa demokrasia ya nchi yetu na ufanisi kwa siasa za CCM,” alisema Heche.
Mbowe Alaani
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akizungumzia hatua ya Methew kuhukumiwa kwenda jela, alisema huo ni
mkakati ulioandaliwa Serikali ya CCM kudhohofisha upinzani na kuwatisha wasifanye siasa.
Hata
hivyo, Mbowe aliwagiza viongozi wa chama hicho nchi zima kuandaa orodha
ya kesi walizonazo ili kuziwasilisha jumuiya za kimataifa kuonyesha
jinsi upinzani unavyokandamizwa na kupokonywa haki yao ya kufanya siasa.
Alisema Methew amehukumiwa wakati tayari Mbunge wa Kilombero, Peter Lijuakali akiwa ameshahukumiwa kwenda jela miezi sita.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment