Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilayani Nzega mkoani Tabora, imemhukumu
kifungo cha maisha Hubasha Ngasa (62) mkazi wa Kijiji cha Ngonho baada
ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka mjukuu wake mwenye umri wa miaka
minne.
Awali Mwendesha Mashtaka wa Jeshi la Polisi, Melito Ukongoji, aliieleza
mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa la kumbaka mtoto huyo Aprili
24 mwaka 2016 baada ya kuachwa na wazazi wake walipokwenda shambani
kulima.
Ukongoji alisema, “Baada ya muda wazazi wa mtoto huyo wakiwa shambani
walisikia kelele za mtoto na walipokwenda kuangalia nini kimetokea,
walikuta tayari mshtakiwa amembaka na kumjeruhi sehemu zake za siri.”
Akisoma hukumu hiyo juzi, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo,
Serafina Nsana, alisema adhabu hiyo imetolewa baada ya mahakama
kuridhika na ushahidi uliowasilisishwa na upande wa mashtaka.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment