Mbunge
wa Nzega Mjini Hussein Bashe amefunga mazito leo asubuhi kuhusiana na
sakata la timua timua linaloendelea dhidi ya wanachama wasaliti ndani ya
CCM huko Jijini Dodoma katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM.
Mbunge
huyo amesema hawezi kuwa na hofu ya aina yeyote kwa kuwa hana jambo
baya alilolifanya ndani ya chama hicho hivyo hawezi kuteteleka na
wanaotimuliwa wanachama.
“Sina
hofu na timua timua ya wanachama wasaliti kwasababau naamini wamefanya
maamuzi kwa kupitia mchakato ndani ya chama, kwa hiyo sina hofu
kwasababu chama chetu kinaongozwa na katiba pamoja na kanuni zilizopo
unakuwa na hofu pale unahisi kuna jambo umelifanya kinyume na
taratibu”-Alisema Bashe
Kwa
upande mwingine Mbunge huyo amegoma kuzungumzia sakata la yeye
kushikiliwa na Jeshi la Polisi hapo jana na kusema suala hilo kamuachia
Katibu Mkuu wa chama hicho ndugu Abdurahaman Kinana.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment