Wabunge Hussein Bashe wa Nzega Mjini na Joseph Kasheku wa Geita wakiwa na aliyewahi kuwa mbunge wa Kisarawe, Adam Malima wamehojiwa polisi na kisha kuachiwa baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kupanga njama za kuvuruga mkutano mkuu wa CCM
Inaelezwa kuwa, wabunge hao ambao ni wajumbe wa mkutano mkuu maalum
wa CCM, ambao unatajiwa kufanyika kesho, Machi 12 mjini Dodoma walikuwa
wakipanga njama za kuvuruga mkutano huo kwa kugawa pesa kwa baadhi ya
wajumbe.
Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma amethibitisha kukamatwa kwa wabunge hao, kwa ajili ya mahojiano, lakini amesema kuwa baada ya mahojiano, wabunge hao wameachiwa kwa dhamana baada ya kujidhamini wao wenyewe.
“Walikuwa wanahojiwa tu lakini kwa sasa wameshaachiwa, kulikuwa na tuhuma kwamba wanagawa hela wanapanga kuvuruga mkutano wa CCM, wamejidhamini wenyewe, na upelelezi bado unaendelea ili kubaini kama ni kweli” Amesema Kamanda Mambosasa
Kuhusu endapo watu hao walikutwa na pesa, Kamanda amesema mmoja kati yao amekutwa na pesa lakini akadai kuwa ni pesa zake kwa ajili ya matumizi binafsi

Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment