Nimeulizwa na watu wengi sana kuhusu tamko la jana la Lipumba
(BWANA YULE) la kuwavua ukurugenzi wakurugenzi wote wa CUF Zanzibar na
kumteua Sakaya kuwa Katibu Mkuu. Nachoweza kuwaeleza ni kuwa; “kichaa
akiiba nguo zako, usikimbizane naye ukiwa hujajisitiri, kavae nguo
kwanza”. Wenye akili na waelewe!
Ukweli ni kuwa Katibu Mkuu wa CUF anachaguliwa na Mkutano Mkuu wa
CUF, kamwe hawezi kuteuliwa na Mwenyekiti wa CUF (hata kama Lipumba
angelikuwa ndiye mwenyekiti wa CUF kama ilivyokuwa zamani).
Pili, wakurugenzi wa CUF wanateuliwa na Mwenyekiti wa CUF kwa
kushauriana na Makamu Mwenyekiti wa CUF. Mwenyekiti wa CUF alijiuzulu
tokea mwaka 2015 na Mkutano Mkuu wa taifa uliidhinisha kujiuzulu kwake
tarehe 21 Agosti 2016, kwa hiyo CUF haina Mwenyekiti kwa sasa. Yupo
mhuni mmoja tu amekalia ofisi na anaishi ofisini kwa kulindwa na dola!
Makamu Mwenyekiti wa CUF alijiuzulu na kujiunga CHADEMA kwa maslahi
ya kitaifa kwenye uchaguzi mkuu na hajachaguliwa mtu mwingine kushika
wadhifa huo.
Kama kuna mtu anasimama hadharani na kufukuza wakurugenzi wa CUF
Bara au Zanzibar hivi sasa, basi mtu huyo si Mwenyekiti wa CUF, labda ni
MSUKULE wa mwenyekiti wa CUF. Itoshe tu kusema kuwa Lipumba anatumiwa
vibaya sana na kama kuna wanasiasa wanatumika basi kwa sasa yeye ana PhD
ya eneo hilo.
Lakini nataka kuwahakikishia watanzania kuwa katika CUF tuko imara
sana, Kamati ya Utendaji ya Taifa inayotambulika ndani ya chama na
iliyothibitishwa na Baraza Kuu ipo na inakutana kila mara, kwa hiyo
kikatiba huwezi kuwa na Kamati nyingine ya utendaji ya taifa isipokuwa
ili iliyothibitishwa na Baraza Kuu ambalo wajumbe wake huchaguliwa na
Mkutano Mkuu.
Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF lipo na linakutana kama
kawaida. Bodi ya Wadhamini ya CUF ipo na imefanya maamuzi mengi hivi
karibuni, ikiwa ni pamoja na kuzifunga akaunti zote za CUF ili
zisiendelee kutumiwa na Bwana Yule kutorosha fedha za chama na kugawana
na genge lake n.k.
Kama nilivyowahi kusema huko nyuma na narudia tena hapa, jeuri yote
ya Lipumba ni CCM na serikali yake, hawa ndio wanamuweka mjini,
anatamba, anaita vyombo vya habari, anatangaza madudu yake n.k.
Lakini kitaalamu tumeshamshinda vita ya ndani, bado ameshikilia
tawi moja tu, CCM na vyombo vya dola – nawahakikishia kuwa tawi hilo
litakatika na Lipumba ataanguka kama mzigo na genge la wahuni wake
litatawanyika kama kondoo wasio na mfugaji na CUF imara itasimama
kuelekea 2020.
Kwa hiyo msitishwe na matamko ya Lipumba na watu wake, ni kweli
watatusumbua sana, lakini tutawashinda tu, na mahali tutakapowashindia
wanapajua na hawana pa kutokea. Hakuna UONGO iliyowahi kuishinda KWELI.
Hakuna WASALITI waliowahi kudumu kwa hiyo nawaomba watanzania
tuendelee kumpuuza kama wanachama wa CUF mkoani Tanga walivyompuuza hivi
karibuni alivyojaribu kufanya ziara mkoani humo. Tumkatae kama wabunge
na madiwani wa CUF walivyomkataa. Tumsuse kama wenyeviti wa mitaa wa CUF
walivyomsusa.
Tuendelee kumzodoa kama anavyozodolewa na familia yake. Let us
disown and continue to neglect him untill CCM registers him officially.
Julius Mtatiro,
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi,
The Civic United Front,
07 Machi 2017.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment