Na,Vero Ignatus ,Arusha.
Mbunge wa
Arusha mjini Godbless Jonathan Lema amefanya mkutano wake wa kwanza
kwa kuzungumza na wananchi wa Arusha baada ya kutoka rumande
alipokuwa ameshikiliwa kwa miezi minne
Akizungumza katika mkutano huo Lema amesema kuwa madiwani wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema watakao kuwa waoga yupo tayari kuwakana mbele ya wananchi na kama hawawezi kuwa majasiri waachanae na chama hicho.
Mkutano
huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiwemo
madiwani wote wa chama hicho katika jiji la Arusha pamoja na wabunge
wa simanjiro na yule wa Monduli.
Aidha
mbunge huyo amesema kuwa yupo kwenye harakati za kukamilisha kukiandika
kitabu chake kitakachotoka hivi karibuni chenye historia ya maisha
halisi ya wafungwa waliopo gerezani bila hatia,sambamba na wale
waliobambikiziwa kesi mbalimbali.
Amewataka
madiwani kuwa sambamba na yeye na kuachana na kauli wanayoisema ya
kuwa wapo nyuma yake kwa kila kitu anachokifanya .
Wapili kutoka kushoto ni mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema
,wakwanza kulia ni mbunge wa Simanjiro James OLemilya akifuatiwa na
aliyeko kulia kwake ni Meya wa jiji la Arusha Kalisti
Lazaro,akifuatiwa na Wema Sepetu,na wakwanza kulia ni mwenyekiti wa
chadema mkoa wa Arusha Derick Magoma
Mbunge
Lema akiwa na Wema Sepetu akisaliamia wananchi wa jiji la Arusha
Mamia
ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo leo jijini
Arusha.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment