Harmonize ameendelea kusisitiza msimamo wake kuwa hajawahi
kusikia kama Diamond na mpenzi wake Jacqueline Wolper waliwahi kuwa na
mahusiano.
Akiongea kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM,
muimbaji huyo amekana kabisa kuwahi kusikia kama mpenzi wake huyo
alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na bosi wake ambaye ni hitmaker wa
Marry You. “I don’t know about that, sijui kama Jackie alishawahi kudate
na Chibu D. Sijui na sijawahi kusikia. Mimi mwanakijiji bro mjini
sijafika siku nyingi, so sijui na sijawahi kusikia ndio kwanza
unanisuprise. Kumbe ilishawahi kutokea hivyo?,” amesema Harmo.
“Confirmation niliyokuwa naihitaji sio hiyo bro, nilikuwa nataka
confirmation kutoka kwa Diamond kwamba anaonaje mimi nikikaa pale kwa
Wolper. Alinijibu kuwa ni mwanamke mzuri lakini hakuniambia kama
alishawahi kudate naye na wala Jackie hajawahi kuniambia kama alishawahi
kudate na Diamond,” ameongeza.
Kwa sasa muimbaji huyo anafanya
vizuri na wimbo wake mpya 'Niambie' ambapo video yake imeshatazamwa mara
571k katika mtandao wa Youtube japo ina siku tano tu tangu ilipotoka.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment