BAADA ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuelezea mafanikio
aliyoyapata, changamoto alizokutana nazo na mipango inayofuata ya mwaka
wake wa pili aliouanza, wanawake wanaofanya biashara ya ‘uchuuzi wa
mwili’ (machangudoa), wameibuka na mbinu mpya ya kumdhibiti kiongozi
huyo ili asiwabughudhi.
Uchunguzi uliofanywa na Risasi Jumamosi umebaini kwamba, baada ya
kuchoshwa na kukimbizwa na kukamatwa na polisi chini ya Kamanda wa
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro wanapojiuza
barabarani kwa amri ya Makonda, sasa wameanzisha mtandao wa kujiuza
ambao unaelezwa ni hatari zaidi.
“Unaambiwa sasa hivi mambo ni kidijitali na ni vigumu kuwakamata kwani
huwezi kumtambua mwanamke anayejiuza kirahisi kwa sababu mchongo mzima
unachongwa mtandaoni kupitia Mitandao ya Kijamii ya Instagram na
WhatsApp na siyo kusimama barabarani kama zamani.
“Wenyewe wanasema wamempiga tobo Makonda kwa kubuni njia mpya ya
kuwaingizia kipato, tena bila kujidhalilisha kama zamani,” alitonya mtoa
taarifa wetu hivyo kutoa ‘asainmenti’ kwa Oparesheni Fichua Maovu (OFM)
ya Global Publishers.
OFM KAZINI Ikiwa kazini, OFM ilitonywa kuwa kwa sasa kuna mbinu mpya
ambayo machangu wanatumia kwa sasa hasa wa maeneo ya Sinza ambao
wametoweka katika vijiwe vyao kisha kujituliza magetoni kwao kusubiria
oda kutoka kwa wanaume hivyo kuwataka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) na polisi kuingilia kati kukomesha ishu hiyo.
“Hivi mnajua kuwa machangu siku hizi hawaonekani kwenye maeneo yao ya
usiku? Unajua kuna kipindi walizidi mno lakini kufuatia udhibiti wa
polisi chini ya Makonda wa kuwapitia na kufunga maeneo, sasa wameunda
magrupu tofautitofauti mitandaoni na kuwavuta wateja wao kirahisi.
WANAFANYAJE? ”
Ishu nzima ipo hivi, wanajitangaza kwa kuanika picha zao za utupu na
nusu utupu pamoja na vipande vya video kwenye Instagram kisha
wanakuwekea namba zao za simu na kukutangazia, ukitaka kujiunga kuwaona
live unatuma kiasi cha kati ya shilingi 5,000 hadi 10,000 na ukiingia
humo unawakuta kibao hivyo TCRA na polisi kazi wanayo.
“Wapo wanaotoa huduma ya kukuunganisha tena kwa utakayemtaka kwa gharama
ya shilingi 10,000 kisha ushindwe mwenyewe tu kwani wapo tu magetoni
wanasubiri uingie kwenye kumi na nane zao,” alisema Abdi, mkazi wa
Afrika Sana, Dar.
OFM YACHIMBA Baada ya kujua mbinu hiyo, OFM ilijipanga na kumtuma
mmojawao ambapo aliingia katika Mtandao wa Instagram na kukutana na
makundi mengi ambayo yamewekwa majina ya kukuonesha kuwa huduma hiyo ipo
kisha akawatumia kiasi hicho cha fedha na punde akaunganishwa na
kushuhudia video na picha za utupu.
MMOJA AINGIA MTEGONI Baada ya kuunganishwa kama yalivyo masharti yao,
aliomba apatiwe mmojawao ambapo aliambiwa atoe tena kiasi kingine cha
shilingi 10,000 na baada ya kufanya malipo hayo aliunganishwa na mrembo
aliyetambulika kwa jina moja la Irene tayari kwa kwenda kujinoma naye.
OFM aliahidiana na Irene kukutana sehemu kwa ajili ya huduma hiyo na
kukubali kufika lakini baada ya kuketi katika maongezi, OFM akiwa katika
harakati za kuchomoa simu apige picha kadhaa, Irene alishtuka na kuwa
mkali kama pilipili ambapo alitaka kumkusanyia watu hivyo OFM kupata
wakati mgumu kabla ya mrembo huyo kutimua kwa kumnyeshea mvua ya matusi.
OFM ARUDI TENA KUNDINI Licha ya Irene kushtuka kama anataka kupigwa
picha, OFM ilirudi tena katika kundi hilo kwa lengo la kumpata mwingine
kwa kuwa alikuwa bado mmoja wa memba hivyo ikawa rahisi kuchukua na
namba ya mwingine lakini kila alipokuwa akipigiwa alipokea na kudanganya
maeneo alipo.
WASIKIE TCRA Baada ya kujiridhisha kuwepo kwa mbinu hiyo mbadala OFM
iliwasiliana na Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy ambaye
alisema kuwa, ishu hapo ni kuwe na mtu wa kwenda kulala kwenye Kitengo
cha Uhalifu wa Kimtandao cha Polisi (Cyber Crime Unity) ambao hao ndiyo
wenye idhini ya kumkamata mtu.
KITENGO CHA CYBER Kuhusu ishu hiyo, kamanda wa kitengo hicho, Mwangasa
Joshua aliliambia gazeti hili kuwa baada ya kupokea malalamiko juu ya
biashara hiyo, jopo lake la uchunguzi litakaa na kuyabaini ‘magrupu’
hayo ili kuyachukulia hatua kwani Sheria ya Makosa ya Mtandao ipo na
inafanya kazi.
TUJIKUMBUSHE Juni mwaka jana, Makonda alitangaza vita na makakapoa
(mashoga) na madadapoa (machangu) walioko jijini Dar kuwa ataendesha
msako mkali wa kuwaondoa, jambo lililofanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Credit - Global Publishers
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment