Serikali ya Kenya pamoja na madaktari nchini humo, hatimaye wametia sahihi makubaliano ya kurudi kazini.
Hii ni baada ya mgomo wa madaktari nchini kenya, ambao umedumu siku mia moja na kuathiri vibaya huduma za afya nchini humo.
Chama cha madaktari kikiongozwa na mwenyekiri wake Oroko Samuel,
kuliungana na waziri wa Afya Cleopha Mailu kwenye ofisi za magavana
wakati wa kutiwa sahihi makubaliano hayo.
Awali kulikuwa na hofu wakati madaktari walikataa kuingia ofisi ambapo
makubaliano hayo yangetiwa sahihi, wakilalamikia utata wa vipengee
fulani.
Madaktari walianza mgomo huo wakidai kuwa serikali imeshindwa kutimiza
makubaliano waliyoafikiana, ya nyongeza ya mishahara yao na kuboreshwa
kwa mazingira ya kufanya kazi.
Wiki iliyopita rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, alitangaza kuwa madaktari wangechukuliwa hatua iwapo hawangemaliza mgomo wao.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment