Mitihani inazidi kumkabili mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) ambaye pia ni kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni, Freeman Mbowe baada ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
kumfungulia kesi yeye na mkewe, Dkt. Lilian Mtei.
Mbowe, mkewe Dkt. Mtui pamoja na Meneja wa Klabu ya Bilicanas, Steven
Mlingo wameitwa mahakamani kupitia barua ya wito iliyotolewa na
Mahakama ya Wilaya ya Ilala.
Mahakama imefanya uamuzi huo baada ya TRA kueleza kuwa imeshindwa
kuwapata ili kuwapa hati ya wito mahakamani huku kesi hiyo
iliyofunguliwa mwaka jana ikiwa imeshatajwa mara nne mahakamani hapo.
Washtakiwa hao waliofunguliwa kesi namba 402 ya mwaka 2016,
wanakabiliwa na mashtaka matatu ikiwa ni pamoja na kutotumia mashine ya
kielektroniki ya EFD kutoa risiti, kinyume cha Sheria ya Usimamizi wa
Kodi ya Mwaka 2015, kutoa nyaraka za uongo na kushindwa kutekeleza
masharti ya sheria tajwa.
Washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kutenda makosa hayo mwezi Mei mwaka jana jijini Dar es Salaam.
Mke wa Mbowe, Dkt. Mtei ni daktari anayefanya kazi katika Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili, lakini mwanasheria wa TRA, Marcel Busegano
aliieleza mahakama hiyo kuwa walifika hospitalini hapo kumpa barua ya
wito bila mafanikio.
Awali, Mbowe aliburuzana mahakamani na Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC) iliyokuwa ikieleza kuwa inamdai zaidi ya shilingi bilioni 1 ya
kodi ya pango iliyokuwepo club ya Billicanas, sakata lililopelekea club
hiyo ya usiku kubomolewa.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment