Kamatakamata
ya wafanyabiashara wa viroba nchini, imesababisha kifo cha
mfanyabiashara maarufu mjini Dodoma, Festo Mselia anayedaiwa kujiua kwa
risasi baada ya kukaguliwa mara mbili na polisi kutokana na kumiliki
bidhaa hiyo.
Kampeni
ya kukamata wafanyabiashara wa viroba nchini, inayosimamiwa na Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) ilianza Machi mosi mwaka huu,
baada ya Serikali kutoa taarifa ya mwisho wa biashara hiyo tangu Mei,
mwaka jana.
Mei
mwaka jana, Serikali ilibainisha kuwa kuanzia kipindi hicho hadi
Januari mosi mwaka huu, ungekuwa mwisho wa kuzalisha biashara ya pombe
kali inayohifadhiwa katika vifungashio hivyo (viroba).
Hata
hivyo, Januari Serikali iliongeza muda hadi Machi mosi ili kutoa nafasi
tena kwa wafanyabiashara waliokuwa na shehena ya vinywaji hivyo
waliofuata taratibu, kumaliza, lakini wengi wamekamatwa wakiwa nazo
katika msako unaoendelea hivi sasa.
Mfanyabiashara
huyo anayemiliki kampuni ya Mselia Enterprises na duka la bia za jumla,
baa na nyumba za kulala wageni mjini Dodoma, alijipiga risasi kwenye
shavu la kushoto juzi, Jumanne akiwa shambani kwake Veyula, nje kidogo
ya mji wa Dodoma.
Daktari
wa zamu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Carolyn Damian
alisema alimpokea Mselia hospitalini hapo akiwa mahututi saa 7 usiku, na
kumweka katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU) na robo saa baadaye
alifariki.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa, Lazaro Mambosasa alithibitisha kupewa taarifa na mtu
kuhusu kusikika kwa mlio wa risasi saa 3 usiku na baadaye saa 5
aliwatuma askari na kwenda kuchunguza na ndipo walipomwona
mfanyabiashara huyo, amejipiga risasi na alikufa kutokana na kutokwa na
damu nyingi.
Mambosasa
alisema baada ya kupewa taarifa, askari walifuatilia eneo ambalo risasi
zilisikika katika shamba la mfanyabiashara huyo eneo la Veyula na
walipofika, waliokota maganda matano ya risasi alizotumia kujiua.
Mfanyakazi
wa mfanyabiashara huyo, Leslie Msigwa alisema ni kweli polisi
walikwenda mara mbili dukani kwake Barabara ya 11, karibu na Ofisi za
TFDA, na mara ya mwisho waliondoka naye akiwa kwenye gari lake prado
likiendeshwa na mteja wao, Mazengo hadi waliposikia kwamba amejiua
shambani kwake, Veyula Dodoma.
Msigwa
alisema ni kweli kwenye stoo yake, kulikuwa na katoni 1,269 za viroba
pamoja na vinywaji vingine, ambavyo huwa wanasambaza katika baa na
maduka mbalimbali.
Msigwa
alisema Ijumaa iliyopita, polisi walifika dukani kwake wakiwa kwenye
magari mawili wakiwa na silaha, wakaingia kukagua ndani na wakaondoka na
wao, wakaenda benki kuweka fedha na kulipia mzigo iliyoagizwa.
Alisema
walimtaka aripoti polisi Jumatatu ya wiki hii na alifanya hivyo na
akarudishwa na polisi dukani na aliingia chumba cha kupumzikia, akalala
hadi saa 1 usiku waliondoka kwenda nyumbani eneo la Area D.
Mfanyakazi
huyo alisema juzi, aliitwa polisi, kila alipopigiwa simu alidai anakuja
hadi ilipofika saa 10 ndipo zilikuja gari za polisi mbili pamoja naye,
akashuka akaingia ndani na baadhi yao wakatoka na kuondoka, yeye
aliwafuata akiwa kwenye prado ikiendeshwa na mteja wake, Mazengo.
Habari
kutoka shambani kwake Veyula, zilisema ni kweli siku ya tukio, Mselia
alikwenda na Mazengo, akamwacha nyuma mahali ilipo mifugo, yeye
akaendelea mbele na walipoona anachelewa, walimfuata na wakaona
amejeruhiwa kwenye shavu.
Msigwa
alisema, yeye na mkewe walipoona anachelewa kurudi, walifunga duka na
wakarudi nyumbani hadi ilipofika saa 2.30, wakaanza kupata taarifa
kutoka kwa ndugu zao kwamba Mselia amejipiga risasi shambani Veyula.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment