Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na
Usimamizi wa Ligi za Tanzania (Kamati ya Saa 72), imemwondoa Mwamuzi wa
kati, Ahmada Simba katika orodha wa waamuzi watakaochezesha mechi za
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu wa 2016/2017.
Hatua hii imefikiwa baada ya utetezi wa
Mwamuzi Simba kudai kwamba hakuona tukio la Mchezaji wa Young African,
Obrey Chirwa ambaye alifunga bao ambalo hata hivyo, mwamuzi alilikataa
na kumwonya mchezaji kwa kadi njano.
Tukio hilo lilitokea katika mchezo ambao
Young Africans walikuwa wageni wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa,
Machi mosi, mwaka huu.
Katika hiyo ya njano ilikuwa ni ya
kwanza kwa Chirwa ambayo hata hivyo kamati ya Saa 72 imeifuta kadi hiyo
kwa mujibu wa kanuni ya 9 (8) baada ya Kamati ya Saa 72 haikupaswa
kutolewa kwa Chirwa kwa sababu hakukuwa na kosa wala mazingira ya
kuonywa.
Kadi hiyo ilikuwa ni msingi wa kadi
nyekundu baada ya Chirwa kufanya faulo ambayo aliadhibiwa tena kwa kadi
ya njano hivyo kutolewa nje kwa mujibu wa taratibu.
Kufutwa kwa kadi ya njano ya kwanza,
kunapelekea kufutwa kwa kadi nyekundu ambayo msingi wa kadi hiyo
ulisababisha kadi nyekundu hivyo mchezaji angempaswa kukosa mchezo
mmoja. Hata hivyo, kadi ya pili ya njano inahesabiwa.
Kadhalika uamuzi mwingine ulikuwa ni
kuipiga faini Young Africans iliyocheza na Simba Februari 25, 2017
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya Wanajwani hao
kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi.
Kitendo hicho ni kwenda kinyume cha
kanuni ya 14 (14) ya Ligi Kuu inayoelekeza kuwa timu zitaingia uwanjani
kwa kutumia milango rasmi. Hivyo kwa kuzingatia Kanuni ya 14 (48) ya
Ligi Kuu, Kamati imeipiga Young Africans fainali ya Sh 500,000 (lakini
tano).
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment