Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye, amesema kama yasemayo kuhusu
elimu ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ni kweli, hamlaumu
kwa maamuzi yake mbalimbali ambayo yamekuwa yakikosolewa vikali na
wananchi.
Akiongea na waandishi wa habari Jumanne hii jijini Dar es Salaam, Sumaye
alidai kuwa Makonda amepewa cheo kikubwa ambacho elimu yake haikimudu.
“Kama ni kweli [Makonda] amefeli darasa la saba kabisa, form four
akafeli zote kabisa, kama ni kweli hivi ulitegemea afanyeje? Aendeshe
mkoa sawa sawa?” alihoji Sumaye.
“Kama hizi failure ni kweli, huo uwezo wa kubeba hata wilaya uko wapi?
Kwahiyo mimi simlamu Makonda. Yule bwana kwenye uongozi kuna kitu
kinaitwa level of incompetency,” ameongeza.
Amedai kuwa huenda katika nyadhifa za chini Makonda alionekana kufanya
vizuri hali iliyopelekea kupandishwa daraja haraka hadi kufikia kwenye
kiwango ambacho hana uwezo nacho.
“Maana kama umefika mahali unavamia vituo vya habari, anakwenda waziri
anayehusika na sekta hiyo anasikitika, anaeleza maelezo yale ambayo
tumeyasikia sisi kwenye mitandao mengine mimi siwezi hata kuyarudia
lazima kuna tatizo.”
Sumaye amesisitiza kuwa Makonda amefika mwisho wa uwezo wake.
Pia Sumaye amemshauri Rais Dkt John Magufuli kutii hisia za wananchi wake katika maamuzi anayoyafanya.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment