Thursday 23 June 2016

Kajala akanusha kutoka kimapenzi na Msami.Fahamu zaidi hapa.

Mwigizaji wa filamu za Kibongo Kajala Masanja amefunguka kuwa msanii wa Bongo Fleva na dansa,Msami ni mshikaji wake tofauti na baadhi ya watu waliokuwa wakidhani kuwa wana uhusiano wa kimapenzi.

‘Unajua kuna watu wanaweza wakawa labda ni washikaji au wana vitu vingi pembeni lakini watu wengine hawajui, mi na Msami ni washkaji sana halafu sio kila siku watu watakuwa wanatuona barabarani au tunapostiana picha kwenye Instagram, lakini mimi na yeye tunaongea vitu vingi kwa hiyo imekuwa rahisi mimi kuacha usingizi wangu kuja kwa Msami, sina uhusiano naye na vitu vingine mtavijua baadae’’ Alisema Kajala.

0 comments:

Post a Comment