Tuesday 14 June 2016

DUNGA ATIMULIWA BRAZIL BAADA YA KUTIA AIBU COPA AMERICA.Fahamu zaidi hapa.

Dunga amefutwa kazi kama kocha mkuu wa Brazil baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya Copa Amerika katika hatua ya makundi.

Dunga ambaye alikuwa nahodha aliyepata mafanikio akiwa na Brazil kwa kuiwezesha kutwaa kombe la Dunia mwaka 1994, alitangazwa kuwa kocha wa timu ya taifa kwa mara ya pili mwaka 2014.

Kikosi cha Brazil kilifungashiwa virago kwenye hatua ya makundi ya michuano ya Copa America kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1987 baada ya kuchezea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Peru siku ya Jumapili.
Dunga, 52, mara ya kwanza alikuwa kocha wa Brazil kuanzia mwaka 2006 hadi 2010, akafanikiwa kushinda taji la Copa America mwaka 2007.

Kocha wa klabu ya Corinthians anapewa nafasi kubwa ya kurithi nafasi iliyoachwa wazi na Dunga.
Kocha huyo mwenye miaka 55 alikiongoza klabu hiyo kushinda taji la ligi kuu ya Brazil (Serie A) mwaka 2011 na  2015, pamoja na Copa Libertadores na World Club Cup mwaka 2012.

Hata hivyo, kocha atakayemrithi Dunga atakiongoza kikosi cha Brazil cha U23 kikiwa na nyota wa Barcelona Neymar kupambana kwenye michuano ya Olympic itakayofanyina Rio de Janeiro, Brazil kuanzia mwezi August.

Mrithi wa Dunga pia atakuwa kwenye wakati mgumu kuhakikisha Brazil inafuzu kucheza kombe la dunia nchini Russia mwaka 2018 kutokana na mwendo wa kusuasua wa kikosi hicho kinachokamata nafasi ya sita kwenye kundi lake katika mbio za kufuzu kwa fainali hizo.

0 comments:

Post a Comment