Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, amesema atapokelea kadi ya Chadema jimboni mwake baadaye mwezi huu.
Kafulila
alitangaza kuhama NCCR-Mageuzi na kurudi Chadema kwa alichoeleza kuwa
ndicho chama kilichojipambanua kuelekea safari ya mabadiliko ifikapo
mwaka 2020.
Kada
huyo tayari amewasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosena
Nyambabe kumjulisha kuwa anajivua uanachama na anarudi Chadema.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi jana, Kafulila alisema ameamua kuwa
atapokelea kadi hiyo jimboni kutokana na mapenzi aliyonayo kwa wananchi
wake.
"Nimepanga
kuchukua kadi mwezi huu jimboni, kwa kuwa ilikuwa nichukue kadi
mwanzoni lakini ilishindikana kutokana na siku kuu, hivyo siku yoyote
kuanzia sasa nitachukua," alisema.
Wakati
anajiuzulu NCCR-Mageuzi na kurudi Chadema, alisema hakufanya uamuzi kwa
kukurupuka bali alitafakari na kushauriwa na wananchi wa jimbo lake, na
kuridhika kurudi huko.
"Nilitafakari
na kushauriwa sana jimboni na kuridhika kwamba Chadema ndiko sehemu
inayojipambanua kwa mikakati ya kuleta mabadiliko yanayotarajiwa na
Watanzania na ni vema kukusanya nguvu ya kila mwenye kiu ya mabadiliko
ndani ya chama kimoja, ili kufupisha safari ya mabadiliko," alisema.
Alipoulizwa
kwa nini amerudi Chadema wakati aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho,
Dk Wilbrod Slaa alipata kumwita sisimizi kwa alichoeleza kuwa hakuwa na
imani naye, alijibu kuwa siasa ni malengo si uhusiano binafsi.
Kafulila
aliongeza kuwa wanasiasa wanaunganishwa na malengo zaidi ya urafiki na
kwamba malengo yake sasa ni kuendelea kupigania mabadiliko ya kimfumo
yanayoenea zaidi kwenye chama hicho (Chadema) kuliko kingine.
Novemba
10, 2009 Kafulila alijivua uanachama wa Chadema na kuhamia NCCR-Mageuzi
kutokana na kuondolewa kwenye nafasi ya uofisa habari wa chama hicho.
Pia
akiwa NCCR-Mageuzi, alitimuliwa uanachama kwa kudaiwa kukiuka taratibu
za chama hicho na tuhuma za kutaka 'kumpindua' Mwenyekiti, James Mbatia.
Hata
hivyo, suala hilo lilipata suluhu baada ya Mbatia kuteuliwa na Rais
mstaafu Jakaya Kikwete kuwa Mbunge. Wakiwa bungeni, Mbatia na Kafulila
walikutana, kuzungumza na hatimaye kumaliza mzozo wao.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment