WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka Wakurugenzi wote wa Halmashauri na
Manispaa nchini kuacha kutoa fedha taslimu na kuwapa madiwani ili
zikafanye kazi za maendeleo.
Badala
yake amewataka waandae mfumo maalum wa kutoa fedha hizo kama
zinavyotolewa fedha za mfuko wa Jimbo ambazo ni maalum kwa wabunge
lakini zinatumika kwa shughuli za maendeleo jimboni.
Ametoa
kauli hiyo jana mchana (Jumatano, Januari 4, 2017) wakati akizungumza
na viongozi na watendaji wa mkoa wa Ruvuma mara baada ya kupokea taarifa
ya mkoa huo kwenye Ikulu ndogo Manispaa ya Songea.
“Nimepata
taarifa kuwa fedha za maendeleo kwa madiwani zinakabidhiwa mkononi.
Hapana. Msiwape fedha mkononi, bali zifuate mfumo wa utoaji fedha wa
Serikali. Kama mlikuwa na matumizi ya aina hiyo, mwisho wake ni jana,” alisisitiza.
“Fedha
za mfuko wa Jimbo ni za Mbunge lakini hapewi mkononi bali zinapelekwa
kwenye Halmashauri na yeye anahusika kwenye kikao cha maamuzi.
Anakubaliana na madiwani wenzake ni miradi ipi ipatiwe fedha, ambayo
mara nyingi inakuwa imekwishaidhinishwa na vikao husika,” aliongeza.
Alisema makusanyo ya fedha yanayofanywa na Halmashauri hayana budi kuangaliwa pia na jinsi fedha hizo zinavyotumiwa.
“Lazima
tukishakusanya tuangalie tumepata kiasi gani, siyo kukaa na kuamua
kutoa sh. laki tano tano kwa kila diwani. Suala la matumizi ni muhimu
sana, ni lazima fedha hizo ziende kwenye miradi ya maendeleo,” alisisitiza.
Alisema
kuna baadhi ya watu wanaamua kugawana fedha kwa kigezo cha maendeleo
lakini wanaishia kutumia fedha hizo kwa kigezo cha kujengeana uwezo
(capacity building).
“Hii
si sahihi na jana nimepiga marufuku posho za aina hii pamoja na fedha
za vitafunwa kwa sababu zinaishia kwa wakubwa wachache na waliozikusanya
hawapati chochote,” aliongeza.
Akizungumzia
kuhusu ukusanyaji wa mapato kwenye Halmashauri, Waziri Mkuu aliwataka
waangalie baadhi ya makampuni ambayo yanajitokeza kutoa vifaa vya
kukusanya ushuru lakini wanatumia software ambazo zinawanufaisha na wao
pia.
“Tumieni
watu wenu wa TEHAMA kukagua mifumo hii kwani kuna baadhi ya watu
wanaoleta zile mashine siyo waaminifu. Watu wa TEHAMA wazikague na
kujiridhisha kuwa hakuna mianya ya wizi. Tumegundua wako wanaokusanya
fedha, lakini asilimia 80 inangia kwenye akaunti za Halmashauri na
asilimia 20 inapelekwa sehemu wanayoijua wao. Ukiangalia unaona mapato
yanaongezeka lakini kumbe pia unaibiwa. Jaribuni kuchunguza na
mjiridhishe na hizo software zao,” alisisitiza.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment