Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Jaji Joseph Warioba amewataka watanzania
wote kuungana na kujiaandaa kukabiliana na baa la njaa ambalo huenda
likatokea, huku akikiri kuwa tatizo la upungufu wa chakula kwa mwaka
huu, ni kubwa kuliko kawaida.
Akizungumza leo wakati akizindua kongamano la 'Wanawake na Uongozi'
katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam, Jaji Warioba amesema
hakuna haja ya watanzania kubishana na kulumbana kama kuna njaa au
upungufu wa chakula, bali kujiandaa ikiwa ni pamoja na kujifunza
kujifunza katika nchi ambazo tatizo hilo limetokea ikiwemo Kenya na
Somalia.
"'Haijalishi kama njaa ipo au kuna upungufu wa chakula kinachotakiwa ni
kuungana na kujiandaa kwa pamoja ili kujua ni jinsi gani tutaweza
kukabiliana na baa la njaa endapo litatokea kama jinsi inavyosemwa,
tujifunze kupitia Kenya na Somalia. Siyo sawa kurushiana maneno huyu
anasema hivi huyu anamjibu vile, tuungane kwa pamoja" Amesema Warioba
ambaye pia alikuwa ndiye Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba a
kuongeza “Serikali ijiandae kukabiliana na njaa kwa sababu ingawa
tumezoea kwamba kila mwaka zipo sehemu zenye upungufu wa chakula, mwaka
huu tatizo ni kubwa”
Kuhusu vita dhidi ya dawa za kulevya, Warioba ametaka elimu itolewe kwa
watu wanaojishughulisha na dawa za kulevya hususani wanaolima bangi
lakini pia wasaidiwe wapate njia mbadala za kuweza kujikimu ili kuachana
na shughuli hizo ambazo zinaathiri asilimia kubwa ya vijana.
Ameongeza kuwa tatizo la dawa za kulevya linaripotiwa kawaida kama siyo tatizo kwa sababu limefanywa kama jambo la siasa.
"Tatizo la dawa za kulevya linazungumzwa kama jambo la kawaida, badala
yake tumetafuta mchepuo wa kisiasa, ambao ndiyo unazungumzwa, Karibu
kila siku utaona taarifa kwamba wameenda askari wameharibu dawa za
kulevya katika mashamba ya bangi, inaripotiwa tu kama tukio halafu
basi.
'Tuseme hapana matumizi ya madawa, madawa ni mengi sana yanayoingia ,
tunajua madhara yake, tuyazuie yanayoingia kutoka nje pamoja na
yanayolimwa, tujitahidi kuwasaidia vijana walioathirika. Tunahitaji
kujenga nguvu za pamoja" Amemalizia jaji Warioba.
Kongamano hilo lililoandaliwa na Mtandao wa Wanawake na Katiba, ni
sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, na limetumika pia
kuzindua kitabu chenye jina 'Nguvu zetu, Sauti zetu, Ajenda katika
mchakato wa katiba mpya' kilichoandaliwa na mtandao huo jijini Dar es
salaam,
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment