SIKU chache baada ya msanii wa kizazi kipya, Ali Kiba, kudai kuwa
anamchukulia mwanamitindo Jokate Mwegelo kama rafiki yake, mrembo huyo
ameibuka na kusema huenda aliteleza kutoa kauli hiyo.
Jokate alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki hii alipokuwa anahojiwa
kwenye kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Clouds Tv, ambapo mrembo
huyo alisema kauli hizo huenda zimetolewa kimakosa.
“Sifikirii sana maana mimi ni mtu ‘positive’ nataka niamini
hawakumaanisha, sasa sijui waliteleza au walikosea,” alisema mrembo huyo
aliyewahi kushika nafasi ya pili kwenye shindano la Miss Tanzania mwaka
2006.
Mrembo huyo alikwenda mbali kwa kusema: “Unajua katika maisha huwezi
kumlazimisha mtu kuona thamani yako, wanasema tenda wema nenda zako
mengine ni matokeo na sipendi kulizungumzia sana maana siku hizi watu
wanapenda sana kuokota maneno wanayatengeneza wanavyojua wao.”
Kiba na mama yake walimkana Jokate kwenye sherehe ya kumpongeza msanii huyo baada ya kurudi kutoka Afrika Kusini na tuzo ya MTV.
Tuzo hiyo ambayo awali alitangazwa Wiz Kid kwamba ndiye aliyeshinda
lakini baadaye uongozi wa MTV wakakiri mshindi halali alikuwa ni Ali
Kiba na kuahidi kumpa tuzo yake nchini Afrika Kusini.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment