Hapa sikutaka kumzungumzia kabisa Makonda hata nilipokuwa Dodoma kwenye
mkutano baadhi ya marafiki tuliosoma nae ushirika tulijadili na kuona
chama kinamlea vibaya sana.
Leo nimeona video ikimuonyesha akivamia ofisi za clouds Tv hili jambo ni
gumu sana sana Mhe. Rais aliangalie kwa kina sana la sivyo linaendelea
kutuchafua sana, ukitazama mitandao ya kijamii utaona tunavyotukanywa na
mtu anayeonekana mbaya ni Rais wangu.
Nemeona mandiko baadhi ya makada wenzangu wabunge na hata mawaziri
wakishanga jambo hili, mimi binafsi nimeshindwa kuvumilia namuomba Rais
wangu na mwenyekiti wangu wa ccm amuondoe Poul Makonda kwenye nafasi hii
ya mkuu wa mkoa kuendelea kumwacha ni kukichafua chama chetu.
Makonda Ondoka Mwanyewe kaka yangu na rafiki yangu ondoka mwenyewe
kuendelea kubaki ni kuifanya ofisi ya Rais inapoteza dira yake na
mwelekeo.
ni mimi
Meijo Laizer
Mjumbe wa NEC TAIFA
Wilaya ya Siha
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment