Ni ukweli usio pingika kwamba asilimia zisizopungua sitini za watanzania
wanaamini kila kitu anachokisema Mange Kimambi kiwe kizuri au kibaya wa
tanzania watakichukua kama kilivyo na watakiamini kwa 100%
Nina uhakika 100% Mange Kimambi akiamua kuliyumbisha hili tukio la
Bashite kwa kuleta information za kumsafisha Bashite ikiwezekana hata
kwa kumchafua Gwajima watanzania watamuamini Mange na shutuma zote
ambazo alikuwa anahusishwa nazo Bashite zitakwisha haraka kama moto wa
nyasi hii yote ni kwa sababu tu Mange ameshika akili watanzania wengi
kiasi kwamba wengine hasa wale wapenda ubuyu ni vigumu sana siku ikapita
bila kupitia IG kwenda kuona Mange kaposti nini.
Na kwa kuwa ma bloggers wengi source yao kubwa ya habari ni kwa Mange na
kwa kuwa watanzania wengi wanategemea habari kutoka kwenye blogs
mbalimbali hivyo basi ina maanisha habari itakayosambazwa itaaminika tu
bila kuchujwa wala nini
Na ukitaka kuamini zaidi kwamba Mange ndio kila kitu ,kuna kipindi
alitulia kidogo kupost habari za Bashite ,kutulia kwa Mange kulififisha
kabisa habari za Bashite watu walikuwa washaanza kumsahau taratibu na
alipoenda kufanya ufunguzi wa barabara alishangiliwa kana kwamba hamna
chochote kinacho endelea juu yake.
Hivyo basi napenda kumalizia kwa kusema kuwa sakata la Bashite litaisha
pale tu Mange atakapoacha kumuongelea watz watalisahau taratibu taratibu
hatimaye wataliacha kabisa
Au kama si kuliacha basi aligeuze juu chini chini juu kwa kutafuta
taarifa za uongo na kweli za kumsafisha Bashite na nina uhakika
atafanikiwa.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment