Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), amesema hana kinyongo
wala uadui na mtu yeyote kuhusu hatua ya serikali kumweka mahabusu
kwenye gereza la Kisongo kwa muda wa miezi 4 kwa kukosa dhamana.
Kauli hiyo aliitoa Jumapili hii mjini Arusha wakati akizungumza katika
ibada ya kwenye Kanisa la Winners Chaple, ambapo alitoa sadaka na
shukrani kwa Mungu na waumini wa kanisa hilo.
Alisema amefurahi kwa sababu Mungu alimpa likizo muhimu kwa kumpendelea
kwa kuwa mbunge wa kwanza kula Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya akiwa
gerezani.
“Nimeomba sana, nimewaombea sana nikiwa gerezani na sikuwa najua nina
uwezo wa kuomba masaa manne ila nimemhubiri Mungu sana gerezani
nimeombea taifa, viongozi, Bunge, Mahakama, Ofisi ya DPP na Rais Dk.
Magufuli,” alisema.
Aliongeza “Ukweli kabisa sina adui kwenye jambo hili na sina kinyongo
kwenye jambo hili, ni mara ya kwanza nilimuona mke wangu akinitetea
gerezani kwa hiyo mimi nilipendelewa kuliko ninyi na hamtakaa mlie
Krismasi gerezani, mkimjua Mungu alivyonibadilisha kupitia gereza
mtatamani muende gerezani,”
Lema aliwaeleza waumini hao kuwa Yusuph alisema wao walimkusudia mabaya
lakini Mungu alimkusudia mema huku akinukuuu andiko lake la shukrani
kutoka katika Biblia kitabu cha Luka 6: 27-28 na kusema kuwa hakuna
mbegu dhalimu inayopandwa itakayovuna rehema.
“Lakini nawaambia ninyi mnaonisikia wapendeni adui zenu,watendeeni mema
wale ambao wanawachukia ninyi, wabarikini ambao wanawalaani ninyi,
waombeeni wale ambao wanawaonea ninyi,” alinukuu kitabu hicho.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment