Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema
taratibu zitafuatwa kuwawajibisha viongozi wake na wa serikali
wanaokabiliwa na tuhuma na madai mbalimbali.
Polepole amesema hayo jana katika Makala ya Kinagaubaga, kipindi
kinachorushwa na Idhaa ya Kiswahili ya Deutschen Welle(DW) baada ya
kuulizwa swali kuhusu chama hicho kulea utovu wa nidhamu wa makada wake,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya
Arumeru, Alexander Mnyeti wanaotuhumiwa kulidhalilisha Bunge na chombo
hicho kwa kauli moja kutaka wajieleze.
Akijibu swali hilo Polepole alisema, “Ninyi hamkujua kama
tutawachukulia watu juzi, Serikali ina utaratibu wake bunge lina
utaratibu wake na chama kina utaratibu wake. Tunao utaratibu tunafuata,
wananchi wawe na subira”
“Wananchi wawe na subira, ninafahamu wananchi wana subira sana,
wasubiri mamlaka za viongozi, hawa wote waliokosea, mchakato wa haki
ufanyike na hatimaye tutaona matunda yake.”
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment