Taarifa mbaya ya kusikitisha kutoka kwa staa wa nyimbo za Injili, Rose
Muhando zinadai kuwa, mwimbaji huyo anasakwa na uongozi wa Sober House
ya Pederef ili waweze kumwokoa kwenye matumizi ya madawa ya kulevya
‘unga’.
Chanzo kilicho karibu na mwanamama huyo ambaye amejijengea jina kubwa
kupitia nyimbo zake nzuri kama Nibebe, kimeeleza kuwa Rose ametoweka
nyumbani kwake mjini Dodoma baada ya kutopea kwenye matumizi ambapo kuna
kiongozi mmoja wa dini ameamua kumsaidia.
“Kuna kiongozi mmoja wa dini hapa Dodoma, ameamua kujitolea kumsaidia
Rose baada ya kusikia hali yake ni mbaya. Ameamua kuwatafuta Pederef ili
wamsake popote alipo na wakimpata wampeleke soba moja kwa moja na
gharama zote yeye atazishughulikia,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupata habari hizo, mwanahabari wetu alimvutia waya Rose ili
kuzungumzia madai hayo ambapo alipopatikana alioomba aachwe kwani
alikuwa kanisani, angempigia mwandishi baadaye.
“Nitakupigia baadaye, nipo kanisani…,” alisikika Rose na kukata simu. Hata alipopigiwa tena baadaye, simu yake haikupokelewa.
Hata hivyo, Wikienda ilimtafuta mmliki wa Sober ya Pederef, Nuru Saleh
aliyekiri kupewa kazi ya kumtafuta Rose na kumfikisha katika soba yao
iliyopo Dodoma na kuanza kumpatia tiba ya kuacha matumizi ya madawa ya
kulevya.
“Ni kweli. Sisi ndiyo kazi yetu. Nimepewa hiyo kazi na kiongozi wa dini,
naomba nisimtaje lakini tumeshaanza kumtafuta na tukimpata tu,
tutampeleka kwenye soba yetu ya Dodoma,” alisema Nuru.
Mara kadhaa Rose amewahi kuripotiwa kuwa anabwia unga lakini mwenyewe amekuwa akikanusha.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment