Mwenyekiti
wa Umoja wa Wanwake Tanzania (UWT), Sophia Simba ametangaza kutogombea
tena nafasi hiyo kwenye uchaguzi wa Chama hicho unaotarajiwa kufanyika
mwaka huu.
Ameyasema
hayo alipokuwa akizungumza na wanawake wa umoja huo wakati wa
maadhimisho ya wiki ya wanawake Duniani yaliyofanyika jijini Dar es
salaam.
“Mimi
Sophia Simba, nimeamua kutogombea kwa hiari yangu mwenyewe nimeamua
kutogombea nafasi ya Mwenyekiti wa Wanawake Taifa UWT katika uchaguzi
ujao,”amesema Sophia Simba.
Sophia
Simba ametaja sababu zilizomfanya asigombee kuwa ni azma yake ya
kuutumikia umoja huo kwa muda wa vipindi viwili tu na si zaidi ya hapo.
Aidha,
amesema kuwa akiwa ndani ya UWT amebahatika kushika nafasi mbalimbali
za uongozi kwa sababu alianzia nafasi ya ukatibu wa tawi la Kaskazini
NDC.
Hata hivyo amesema kuwa anamshukuru mungu kwa kumjalia kushika nafasi mbalimbali kwa kuwa amekuwa mbunge kwa muda wa miaka 22.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment