HAMNAZO! Msanii muuza sura katika video za Bongo Fleva, Zena Abdallah
‘Jike Shupa’ ametoa kali ya mwaka baada ya kudai haogopi Ukimwi kwa kuwa
ni ugonjwa wa kawaida, ndiyo maana amekuwa akibadili wanaume ovyo bila
wasiwasi.
Aliiambia safu ya Za Motomoto News kuwa wanaume wengi wamekuwa
wakimtokea na kumhitaji kimapenzi, hivyo kutokana na uwingi wao,
anajikuta akishindwa kuwakatalia wote hivyo kuwakubalia, pamoja na
ukweli kuwa humpa fedha.
“Sioni shida kubadili wanaume kila siku maana wao wenyewe ndiyo
wanaonitamani, siogopi Ukimwi maana kila mtu duniani ameathirika, huo ni
ugonjwa wa kawaida kama mwingine, wanaume wanaonitamani ni wengi hivyo
nashindwa kuwakataa, naingia nao kwenye uhusiano siku mbili tatu
tunaachana, nakuwa na mwingine,” alisema Jike Shupa.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment